Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Muongozo wa elimu kwa maendeleo endelevu kwa mwaka 2023/2030 wapitishwa

Arusha. Serikali imepitisha Mpango wa kitaifa wa muongozo wa elimu kwa maendeleo endelevu kwa mwaka 2023 / 2030 yenye lengo la kuwaandaa wanafunzi kuelewa mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuwaandaa katika masuala ya kilimo, viwanda na ujasiriamali.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameyazungumza hayo Jijini Arusha kwenye hafla ya utiaji saini wa kupitisha mpango wa kitaifa wa elimu kwa maendeleo endelevu.

Waziri Mkenda amesema nchi za SADC zilikutana wakaona kwamba UNESCO ifanye kazi ya kuratibu muongozo huo kwa nchi za SADC lengo ni kuona kuwa elimu wanayotoa inawaandaa vijana katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi na masuala ya mazingira kwa.

Amesema ni vizuri suala hilo likawa ni sehemu ya elimu ambayo wanatoa na wanaangalia masuala ya kilimo, viwanda na uwekezaji ili elimu inayotolewa sasa hivi iweze kuwaandaa vijana katika mambo ya kilimo, viwanda na ujasiriamali.

"Tunashukuru sana UNESCO na SADC kwa masuala mbalimbali ambayo wameyafanya katika maandalizi haya ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya nchi yetu," amesema Mkenda 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar, Salum Abdullah ameeleza kuwa muongozo huo unasisitiza zaidi kuwapatia vijana elimu itakayomjenga kutumia ujuzi atakaoupata shuleni katika kutatua changamoto za kijamii na kumletea maendeleo ya kiuchumi.
Abdullah amesema mpango huo ni utekelezaji wa elimu kwa maendeleo endelevu ambapo ni agizo la umoja wa mataifa kuwa kila nchi iweze kuwa na mpango huo kwa ajili ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030.

Ameongeza kwa kusema Zanzibar imekuja wakati muafaka kwani sasahivi wanafanya maboresho ya mitaala ya elimu kuhakikisha wanafunzi wanatumia uelewa walioupata kwa ajili ya kutatua changamoto zake mbalimbali na kwa  maendeleo ya kiuchumi. 

Nao baadhi ya wadau mbalimbali waliupongeza mpango huo kwani utasaidia kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu na kuweza kuwawezesha vijana kujiajiri na kuondokana na changamoto ya ajira.