Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtumbwi wazama Kisiwa cha Rukuba, watatu wahofiwa kufa

Muktasari:

  • Watu watatu wananahofiwa kufariki dunia huku mmoja akinusurika baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuvua dagaa kuzama ndani ya Ziwa Victoria wakati wakiendelea na shughuli zao.

Musoma. Watu watatu akiwemo Katekista wa Kanisa Katoliki Parokia Teule ya Rukuba iliyopo wilayani Musoma mkoani Mara, wanahofiwa kufariki dunia baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kwa ajili ya uvuvi kuzama Ziwa Victoria katika Kisiwa cha Rukuba.

Akizungumza kwa njia ya simu leo Jumanne Aprili 22, 2025, Mwenyekiti wa Parokia hiyo, Jovin Mafuru amesema Katekista huyo pamoja na wenzake watatu walikwenda ziwani kwa ajili ya kuvua dagaa.

Amesema wakiwa wanaendelea na shughuli zao tufani kubwa ilipiga mtumbwi na kuzama majini hali iliyosababisha wavuvi hao wanne kuzama majini kabla ya mmoja kufanikiwa kujiokoa.
Amemtaja Katekista huyo kuwa ni Cleophace Mganga (45) Mkazi wa Kisiwa cha Rukuba na kwamba jitihada za kuwatafuta bado zinaendelea.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere amekiri kuwepo kwa tukio hilo huku akiwataja watu wengine wanohofiwa kufariki dunia kuwa ni pamoja na Frederick Ibaso (39) na Revocatus Ntega (35).

"Walikuwa wanne kwenye mtumbwi wakiwa wanaendelea na shughuli zao walipigwa na dhoruba mtumbwi ukazama na wao wakazama pia ila mmoja wao aliweza kujikoa na kutoa taarifa juu ya tukio hilo," amesema.

Amemtaja aliyenusurika katika tukio hilo lililotokea usiku wa Aprili 21, 2025 kuwa ni Makebe Buriro (22) ambaye alifanikiwa kuogelea kisha kukaa kwenye maboya yaliyotengenezwa na matete na kuendelea kuelea juu ya maji.

"Akiwa anaelea kuna mtumbwi mmoja ulipita akaokolewa lakini wenzie hadi sasa bado hawajapatikana, shughuli za uokozi bado zinaendelea katika eneo hilo ingawa zipo changanoto kadhaa," amefafanua.

Amesema moja ya changamoto inayowakanili waokoaji ni pamoja na umbali wa eneo la tukio hadi nchi kavu ambapo ni mwendo wa takriban saa 2 na kwamba hali hiyo imesababisha waokoji kuchukua muda mrefu kufika eneoe la tukio hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa mawimbi ni makubwa ziwani kulingana na hali ya hewa.

Magere ametoa wito kwa wavuvi na wale wote wanaotumia usafiri wa majini kuwa makini nyakati hizi za mvua huku akiwataka kufuatialia utabiri wa hali ya hewa pamoja na kuvaa majaketi ya uokoaji muda wote wanapokuwa majini.