Mtuhumiwa wa mirungi aliyeachiwa, asomewa shtaka upya

Muktasari:
- Mkazi wa Mlandizi Mohamed Issa (29) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi (Catha edulis Khat) zenye uzito wa kilo 302.15.
Dar es Salaam. Mkazi wa Mlandizi Mohamed Issa (29) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi (Catha edulis Khat) zenye uzito wa kilo 302.15.
Wakili wa Serikali, Judith Kyamba akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amir Msumi kuwa Julai 21, 2019 katika eneo la Kiwalani, wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam mshtakiwa huyo alikutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilo 285.89.
Katika shtaka la pili inadaiwa kuwa Julai 25, 2019 katika ofisi za Posta Mtaa wa Azikiwe, Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Mohamed alikutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilogramu 16.26.
Judith alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, wanaendelea na mchakato wa kuwasilisha taarifa muhimu kwa ajili ya kwenda Mahakama Kuu.
Hakimu Mkazi Msumi alimtaka mshtakiwa huyo kutojibu chochote kuhusiana na shtaka linalomkabili Kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.
Kesi hiyo itarudi tena Septemba 14, 2023 kwa ajili ya kutajwa.
Awali mshtakiwa huyo alidai kuwa kesi hiyo siyo mpya na alishasomewa mahakamani hapo mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Augustino Mbando na upelelezi wake ulikamilika bapo shauri lilipelekwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
"Baada ya kupelekwa katika mahakama hiyo walisikiliza shahidi wa kwanza, ndipo Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hii, nikaachiwa na kukamatwa tena.