Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoto mchanga atoweka nyumbani, polisi waanzisha uchunguzi

Mama wa mtoto mchanga aliyetoweka akiwa ndani ya nyumba waliyo kuwa wakiishi Kata ya Iyela jijini Mbeya Neema Mkuywa(28), akiwa na baadhi ya majirani.

Muktasari:

  • Tukio la kutoweka kwa mtoto huyo lilitokea Aprili 29, 2025, katika Kata ya Iyela jijini Mbeya, akiwa amelazwa kwenye kochi sebuleni.

Mbeya.Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeanzisha uchunguzi kufuatia tukio la kutoweka kwa mtoto mchanga mwenye umri wa siku 10, lililotokea katika Kata ya Iyela, jijini Mbeya.

Tukio hilo liliripotiwa Aprili 29, 2025, muda mfupi baada ya mama wa mtoto huyo, Neema Mkunywa (28), kutoka nje kumsindikiza mgeni huku akiwa amemlaza mtoto wake sebuleni juu ya kochi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, amezungumzia tukio hilo jana Mei 3, 2025 na kuwa uchunguzi wa awali umeanza kufanyika ili kubaini waliohusika.

"Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini mtu au watu waliohusika katika tukio hili. Taarifa za awali zinaeleza kuwa mama wa mtoto huyo alikuwa na mgeni ambaye alimsindikiza umbali wa takriban mita 600, na aliporejea hakumkuta mtoto wake," alisema Kamanda Kuzaga.

Aliongeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kuelewa mazingira halisi ya kutoweka kwa mtoto huyo, huku akitoa wito kwa wazazi kuwajibika katika ulinzi wa familia, hasa kwa watoto wachanga wasioweza kujilinda.

Akielezea tukio hilo leo Jumapili Mei, 2025, mama wa mtoto huyo ameiambia Mwananchi kuwa mtoto huyo ni wa kwanza kwake na alijifungua kwa njia ya upasuaji.

Amesema alipata ugeni wa dada yake aliyekuja kumjulia hali na baada ya kuondoka, alimuacha mtoto kwenye kochi na kwenda kumsindikiza.

"Niliporudi sikumkuta mtoto, nikamuuliza mwenye nyumba kama ameona mtu aliyeingia na kutoka na mtoto, lakini alikataa kuwa na taarifa. Baada ya hapo tulitoa taarifa kwa serikali ya mtaa kwa hatua zaidi," amesimulia Neema.

“Baadaye tulienda kituo cha polisi kutoa taarifa, lakini juhudi za kumtafuta mwanangu  hazijazaa matunda mpaka sasa,” amesema.

Neema ametoa wito kwa Jeshi la Polisi na Watanzania kwa ujumla kumsaidia ili mwanawe apatikane salama.

Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa wa Iyela, Gabriel Button amesema tukio hilo limemsikitisha kwa kuwa ni la kwanza kutokea katika mtaa huo.

Amesemja baada ya kupata taarifa walishirikiana na wananchi kutoa taarifa kwa polisi na kuandaa mkutano wa hadhara, waligawanyika katika makundi kumsaka mtoto huyo bila mafanikio.

"Wazazi msimame imara katika malezi na ulinzi wa watoto wenu. Tuwe waangalifu na tusiamini wageni kirahisi, ili kuepuka matukio ya aina hii," amesisitiza.