Mtanzania ateuliwa UNEP

Elizabeth Mrema
Muktasari:
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), amemteua Elizabeth Mrema, ambaye ni raia wa Tanzania kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira (UNEP).
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amemteua Elizabeth Mrema wa Tanzania kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mazingira (UNEP).
Elizabeth anachukua nafasi ya Joyce Msuya ambaye pia anatoka Tanzania aliyeuteuliwa kushika wadhifa huyo mwaka 2018.
Kabla ya uteuzi huo, Mrema alikuwa Katibu Mtendaji wa Shirika la UN Biodiversity.
Msuya aliteuliwa kuiongoza UNEP akichukua nafasi ya Ibrahim Thiaw wa Mauritania, ambaye alimaliza muda wake wa kuhudumu.
Hadi anateuliwa katika nafasi hiyo mpya, Msuya alikuwa mshauri wa Makamu Rais wa Benki ya Dunia (WB) kwa ukanda wa Asia Mashariki na Pacific jijini Washington, DC wadhifa alioushikilia tangu mwaka 2017.
Pia, Msuya alisihika nyadhifa mbalimbali katika ngazi ya uandamizi kwenye Benki ya Dunia ikiwemo mwakilishi wa Benki ya Dunia na Mkuu wa ofisi ya benki hiyo hiyo Korea Kusini na mratibu wa taasisi ya Benki ya Dunia inayosimamia Asia Mashariki na Pasifiki nchini China