Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtanzania ahukumiwa kunyongwa Uganda

Kampala. Mahakama Kuu ya Uganda, imemhukumu raia mmoja wa Tanzania kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji.

Mtanzania huyo aliyetambuliwa kwa jina la Matule Chresporeto Coleheri, mkazi wa Bukoba anadaiwa kumuua mfanyakazi mwenzake katika shamba moja lililoko eneo la Wakyuto wilayani Nakaseke.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Steven Mubiru alisema baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka, Mahakama imejiridhisha kuwa Matule ndiye aliyetenda kosa hilo.

Alisema mashahidi watatu walioshuhudia tukio hilo wameiridhisha Mahakama kuwa Thomas Kamuhebwa aliuawa na mtuhumiwa huyo. Mwili wa Kamuhebwa ulikutwa ukiwa umetupwa katika shimo na kufungwa katika begi na uliokotwa karibu na makazi ya mshtakiwa.

Hata hivyo, mbele ya Mahakama hiyo, Matule alijitetea kutohusika katika mauaji hayo na kudai tuhuma hizo zilitengenezwa na watu waliotaka kuiba magogo yake aliyoyaandaa kwa ajili ya kuzalisha mkaa.

Awali, ilielezwa mahakamani hapo kuwa Matule ni mhamiaji kutoka Tanzania aliyekuwa akifanya kazi za vibarua na kwamba Februari 6, 2014 alimuua Kamuhebwa kwa sababu zisizojulikana na kufukia mwili wake katika shimo.