Mradi wa umwagiliaji Mbulu wa Sh6.4 bil waanza utekelezaji

Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Mbulu, Yefred Myezi (kushoto) akiwa eneo la mradi wa skimu ya umwagiliaji Kijiji cha Tlawi wilayani humo ambao unatekelezwa na Serikali kwa gharama ya Sh6.4 bilioni. Picha na Mohamed Hamad.

Muktasari:

  • Wananchi elfu 14,000 Kijiji cha Tlawi kata ya Tlawi Mbulu Mji kunufaika na skimu hiyo itakayoanza na hekta 100.

Mbulu. Wananchi wa Kijiji cha Tlawi, Kata ya Tlawi wilayani Mbulu mkoani Manyara, wataondokana na changamoto ya maji, sambamba na kuwa na uhakika wa chakula baada ya kukamilika skimu ya umwahiliaji iliyoanza Feb mwaka 2023.

Serikali ya awamu ya sita imetoa Sh6.4 bil kwa ajili ya ujenzi wa skimu ya umwagiliaji Kijiji cha Tlawi ambao awali walikuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji pamoja na chakula vha uhakika.

"Mradi huo ni wa miezi kumi, ulianza Feb 15, 2023 na uko katika hatua za mwanzo, utakuwa na lita laki tatu na elfu themanini, mkandarasi na vifaa wako kazini mpaka wakiendelea na ujenzi wa skimu hiyoya umwagiliaji Tlawi" amesema Yefred Myenzi ambaye ni Mkurugenzi Mbulu Mjini.

Akizungumza hayo hii leo Machi 19, 2023 Mkurugenzi wa Mbulu Mji, Yefred Myenzi amesema, alipokea 6.4 bil za Skimu ya Umwailiaji Kijiji cha Tlawi kata ya Tlawi zilizotolewa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwaondolea adha wananchi kuwa na kilimo vha uhakika.

"Kijiji cha Tlawi Mwezi Februari mwaka huu Serikali imetoa kiasi cha Sh6.4 bilioni za mradi mkubwa wa ujenzi wa skimu ya umwagiliaji kwa ajili. Mradi huu ulianza rasmi vifaa kama magreda, matingatinga yako ya kutosha na shughuli zinaendelea za ujenzi hapa kama unavyoona mwandishi," amesema Myenzi.

Wale watakaofika hapa mwaka ujao 2024 bonde hili watalikuta likiwa lina mazao mengi yakutosha, shughuli za umwagiliaji zinaendelea kama kawaida, maji yatakuwa mengi kiasi cha kutosha na kuongeza pamoja na mambo mengine Serikali ya awamu ya sita imeiona Mbulu mji imetoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo.

Mhandisi Richard Mgaya wa Skimu ya umwagiliaji Mbulu akizungumzia mradi huo alisema Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetoa kiasi cha Sh6.4 bil ili wananchi wa Kijiji cha Tlawi wawe na uhakika wa maji kwa ajili ya shughuli za kilimo cha umwagiliaji

"Skimu hii itahusisha ujenzi wa bwawa litakalokuwa na lita laki tatu na themanini. Pia kutakuwa na miundombinu ya umwagiliaji ikitokea kwenye bwawa hadi mashambani ambako kutakuwa na mifereji ya maji, pia kutakuwa na ujenzi wa ofisi ya meneja wa mradi ambayo itatumiwa pia na chama cha umwagiliaji na skimu ya Tlawi," amesema Mhandisi Mgaya.

Mtaalamu wa Kampuni ya SIETCO, Luujing kum   akizungumza na Mwananchi Digital amesema watekeleza mradi huo kwa kiwango bora na cha hali ya juu ili mradi huo uwe na tija kwa wananchi hao.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Tlawi, Joakimu Gabriel ameeleza kukamilika kwa mradi huo kutasaidia wananchi hao kuwa na uhakika wa chakula sambamba na upatikanaji wa maji tofauti na ilivyo sasa. Mwenyekiti wa mradi wa Skimu ya Umwagiliaji Tlawi, Wilfred Obay amesema mbali na kilimo cha mahindi watalima pia vitunguu viazi pamoja na mboga mboga.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Tlawi, Anton Genda ameshukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi hao mradi huo utakapokamilika utakuwa na manufaa makubwa kwao.

Hata hivyo sasa wana changamoto ya kilimo cha kutegemea mvua ambacho hakina uhakika hivyo wakulima hao hupata hasara na mradi utakapokamilika wataondokana pia na umaskini wa kipato.