Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpango akemea wizi wa dawa za Serikali

Muktasari:

  • Mkutano mkuu wa 55 na Kongamano la Kisayansi la mwaka la Chama cha Wafamasia Tanzania (PST), unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha, ukiwa na kaulimbiu isemayo ‘Famasia kiini cha afya kwa wote, ubunifu, uwekezaji na afya jumuishi kwa wote’.

Arusha. Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango amekemea wizi wa dawa za Serikali unaosababisha upungufu wa dawa katika vituo vya afya, akiagiza watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo wachukuliwe hatua stahiki.

Dk Mpango ameyasema hayo leo Jumatano Juni 4, 2025 akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 55 na Kongamano la Kisayansi la mwaka la Chama cha Wafamasia Tanzania (PST), linalofanyika jijini Arusha.

Amesema kuwa licha ya Serikali kutumia fedha nyingi katika ununuzi wa dawa bado kuna wizi mkubwa na upotevu, ambazo badala ya kupatikana kwenye vituo vya afya zinapatikana kwenye maduka binafsi ya dawa.

Amekemea wizi na upotevu huo wa dawa unaosababisha kukosekana kwa bidhaa hiyo muhimu katika vituo vya afya.

"Ninasikitika kusema baadhi ya maduka yanamilikiwa na baadhi yenu, hili jambo halikubaliki na linafifisha juhudi za Serikali katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi.”

"Kwa hiyo kupitia jukwaa hili ninawataka wale wote wanaojihusisha na tabia hii waache, kwa kuwa masikio ya vyombo yapo hapa, lakini pia vyombo vya habari basi wale wanaohusika wachukuliwe hatua stahiki kwani wanaturudisha nyuma," ameongeza.

Dk Mpango amesema, upatikanaji wa dawa ni kigezo muhimu katika kupima utendaji wa Serikali ambapo kila mwezi zinatumika Sh17 bilioni, kwa ajili ya ununuzi wa dawa jambo linalosababisha upatikanaji vituoni kuwa asilimia 89.

Amewasisitiza wanataaluma hao kufanya kazi kwa kuzingatia kiapo na miiko ya taaluma hiyo na kulitaka Baraza la Taifa la Famasia kulisimamia kwa ukaribu suala hilo, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Kuhusu elimu ya matumizi sahihi ya dawa, Dk Mpango amesema, "yamekuwepo matumizi yasiyo sahihi ya dawa kwa baadhi ya wananchi wetu, ikiwemo matumizi ya dawa pasipo kushauriwa na daktari, matumizi ya dawa za usingizi kutumika kama kilevi, kutumika kukoleza pombe za asili. Ninawasihi muendelee kutoa kipaumbele kwa suala la elimu ya matumizi sahihi ya dawa ili jamii iepuke matumizi holela," ameongeza.


Uchaguzi

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Dk Mpango amewataka Watanzania kutoingia kwenye mkumbo wa kufanya kampeni za vurugu au kutukanana na kuwa hiyo siyo jadi ya Mtanzania.

"Bila amani hakuna wafamasia wala shughuli nyingine yoyote itakayofanyika, bila amani hata viongozi wetu wa dini wanaotuombea hawataweza kufanya kazi hiyo," amesema.

Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Grace Magembe  amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 tayari wameshapokea Sh166.7 bilioni ambayo ni sawa na asilimia 83.3 ya bajeti ambayo waliidhinishiwa kwa mwaka wa fedha ambao bado haujaisha.

Aidha amewataka wataalamu hao kutekeleza majukumu yao, kwa maadili ya kazi yao ikiwemo kutoa huduma bora za dawa kwa wananchi.

Awali rais wa PST, Fadhili Hezekiah aliiomba Serikali kutoa kipaumbele cha ajira za wafamasia na kuboresha muundo wa utendaji katika hospitali za kuanzia ngazi ya Taifa, kanda na mikoa, ili kupata wakurugenzi wa tiba wenye sifa stahiki.

Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Grace Magembe amewataka wataalamu hao kutumikia wananchi kwa weledi na kuzingatia maadili yao ikiwemo kutoa huduma bora ya dawa kwa wananchi.

"Tutaendelea kufanya kazi kwa uadilifu tukizingatia kipaumbele chetu ambacho ni mahitaji ya wananchi. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema mkoa huo unatarajia kupokea kambi ya madaktari bingwa itakayoanza Juni 23 hadi 29 mwaka huu, ikiwa ni mwendelezo wa kliniki ya madaktari bingwa iliyofanyika mwaka jana.

"Mwaka jana tulihudumia watu zaidi ya  32,000 wengi wao hawakuwa na uwezo wa kulipa gharama za matibabu, wakarudi nyumbani wakiwa wanamlilia Mungu wao na sauti zile zilimfikia na hatimaye tukafanya na leo natumia fursa hii kuwaambia wananchi wa Arusha kwamba, kambi ile itafanyika tena mwezi huu," amesema.