Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mmoja auawa, 8 wajeruhiwa na watu wasiojulikana

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mbaraka Batenga akiwajulia hali majeruhi nane waliolazwa Hoapitali ya Kiteto. Picha na Mohamed Hamad Kiteto.

Muktasari:

  • Mkuu wa Wilaya ya Kiteto amethibitisha kutokea kwa tukio la mtu mmoja kuuawa na wengine nane kujeruhiwa baada ya kuvaamiwa wakiandaa shamba kwa ajili ya kilimo.

Kiteto. Mkulima mmoja ambaye jina lake halikufahamika ameuawa na wengine nane kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Septemba 11, 2023 wakidaiwa kuandaa mashamba eneo la hifadhi ya Emboley Murtangas.

Serikali wilayani Kiteto imesema eneo lililosababisha mgogoro huo sio la kilimo na kwamba waliosababisha mgogoro huo ni watu kutoka nje ya wilaya hiyo ambao wamevamia eneo hilo kinyume na mipango ya matumizi ya ardhi ya kijiji husika.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mbaraka Batenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo baada ya mtu mmoja kuuawa na wengine nane kujeruhiwa na watu wasiojulikana huku majeruhi wakilazwa katika hospitali ya wilaya ya Kiteto kwa kwa ajili ya kupewa matibabu.

"Hili eneo sio la kilimo kuna mtu kutoka alikotoka taarifa nilizo nazo mwenye eneo la mgogoro ametokea Dar es Salaam akaja kutumia eneo hilo kwa kilimo.

Kwa bahati mbaya sana ni mtumishi wa umma ambaye anafahamu taratibu angeweza kufuata taratibu za kupata eneo ambalo liko salama zaidi lakini tunao watu wanatoka nje ya wilaya wanakuja huku ama kwa kudanganywa ama kwa wao kuingia kwa kificho wanakamata maeneo na kutuletea migogoro kama ilivyotokea leo," amesema DC Batenga.

DC Batenga amesema kuwa hilo eneo limeshatokea tatizo mhusika mwenye eneo hilo tunamtafuta atapatikana tu na atachukuliwa hatua kwa sababu lilipo sio eneo la kilimo na ameingia kwa jinai na kusababisha matatizo.

"Mimi nishukuru hata hawa majeruhi wanaendelea vizuri na nitoe masikitiko yangu kuwa kuna mmoja amepoteza maisha kama watu wangefuata sheria na taratibu tusingeweza kufika huko na wanaotufikisha hapa ni wanaotokea nje ya Wilaya ya Kiteto na kuja huku kutumia maeneo kinyemela kupitia viongozi ama kupitia wananchi wengine," amesema.

Kwa upande wa majeruhu hao wamezungumzia namna walivyonusurika kifo wakisema baada ya kuvamiwa na kundi kubwa la watu usiku wa manane walitimkia porini na waliobaki ndio waliojeruhiwa na mwenzao mmoja kuuawa.

"Baada ya kusikia watu wamevamia hapo tulipokuwa tumelala, wakiongea lugha ya kimasai walianza kuvunja kibanda na kuingia ndani na kuanza kushambulia watu wa rungu na mapanga," amesema Emmanue Shayo majeruhi.

"Nilikimbilia porini kutokea ndani ya kibanda baada ya kuona watu wanapigwa fimbo na kukatwa mapanga mwenzetu mmoja amepoteza maisha na wenzangu wengine nane wamejeruhiwa baada ya kupigwa na wamelazwa hapa hospitali ya Kiteto.

Naye Kibereka Lameck majeruhi hao amesema walifika hapo kuandaa mashamba kung'oa visiki hivyo kilichotokea ni kuvamiwa na watu hao na kuwajeruhi huku wakiwa wamemuua mwenzao.

"Hawa waliotuvamia walikuwa wengi sana ni kama walijiandaa na kuja kufanya mauaji hapa walikuwa ni wamasai wao hawapendi makabila mengine hapo  wakalime katika maeneo hayo lakini mle hata wao wanalima," amesema Lameck.