Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wabunge wataka chombo cha kutatua migogoro Sadic

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile

Muktasari:

  • Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeishauri mambo mbalimbali kuhusu azimio la itifaki ya biashara na huduma ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) yaa Mwaka 2012.

Dodoma. Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeishauri kuundwa chombo maalum cha kutatua migogoro, mara baada ya kuridhia azimio la itifaki ya biashara na huduma ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) ya Mwaka 2012.

Hayo yalisemwa leo Agosti 31, 2023 na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mariam Ditopile wakati akiwasilisha maoni ya Bunge kuhusu azimio hilo.

Ameshauri kuundwa kwa chombo cha kutatua migogoro kwa sababu ufanyaji wa biashara mara nyingi huwa na migogoro inayohusisha ushuru na vikwazo visivyokuwa vya kiushuru.

“Kamati inashauri kwamba ni muhimu kuanzisha chombo kitakachosimamia masuala ya utatuzi wa migogoro ya kibiashara, mara tu baada ya itifaki kuanza kutekelezwa, badala ya kusubiri hadi mgogoro utakapoibuka,” amesema.

Pia amesema kwa kuwa ipo changamoto ya madereva wa malori kuzuiliwa kupita katika baadhi ya mipaka ya nchi za Sadc, hali inayopelekea bidhaa kuharibika.

“Kamati inaiomba Serikali kuhakikisha changamoto hii inatatuliwa ili isiwe kikwazo kwenye utekelezaji wa itifaki ya biashara ya huduma,” amesema.

Aidha, Mariam ameshauri kuboresha usimamizi katika sekta zinazohusu biashara za huduma na kuimarisha miundombinu ya mawasiliano.