Mke wa Sabaya amaliza kutoa ushahidi kesi ikiahirishwa kwa muda

Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi akiwemo aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wakizungumza na Mawakili wanaowatetea katika kesi hiyo (Picha na Janeth Mushi).
Muktasari:
Mke wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, Jesca Thomas amemaliza kutoa ushahidi leo Januari 18, 2022 baada ya kumaliza kuulizwa maswali ya dodoso na jopo la Mawakili watano wa Jamhuri.
Arusha. Mke wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, Jesca Thomas amemaliza kutoa ushahidi leo Januari 18, 2022 baada ya kumaliza kuulizwa maswali ya dodoso na jopo la Mawakili watano wa Jamhuri.
Jesca ambaye ni shahidi wa pili wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2021 inayomkabili Sabaya na wenzake sita alianza kutoa ushahidi jana katika kesi ambayo inaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa upande wa washitakiwa kujitetea.
Baada ya shahidi kumaliza ushahidi wake Wakili wa utetezi Mosses Mahuna aliielza mahakama kuwa shahidi anayefuata ni mtuhimiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Sabaya ambaye anaanza kujitetea.
Hakimu Patricia Kisinda anasema anaahirisha kesi kwa dakika tano kisha mahakama kurejea.
Jana Jumatatu akiongozwa na Wakili Mosses Mahuna anayemtetea Sabaya, Jesca alijitambulisha mahakamani hapo kuwa ni mke wa mshitakiwa huyo na walifunga ndoa mwaka 2018.
Hata hivyo jana Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofmed Mtenga hakumaliza kumhoji shahidi ambapo kesi iliahirishwa mpaka leo ambapo mahojiano yaliendelea.
Hapa ni sehemu ya muendelezo wa maswali ya dodosoa ya Wakili Ofmed Mtenga na shahidi;
Wakili: Unaelewa maana ya kuapa mhkmn kabla ya kutoa ushahidi
Shahidi: Naelewa
Wakili: Unaelewa ukisema uongo mahakamani unaweza ukafunguliwa kesi ukafungwa miaka 5
Shahidi: Naelewa
Wakili: Hebu tutajie ile namba ambayo ulisema ulikuwa unatumia 22.1.2021
Shahidi: 0758 707171
Wakili: Wewe hujawahi kuisajili hii namba
Shahidi: Ndio
Wakili: Lengai Ole Sabaya ndiye aliyesajili
Shahidi: Ndio
Wakili: Na pia tutajie namba ya gari ile ambayo ulisema unaendaha ile VX masai
Shahidi: T 341 ANT
Wakili: Na ulisema hii gari ulinunua baada ya kuanza kuiahi na Sabaya
Shahidi: Ndio
Wakili: Mlinunua Sh ngapi?
Shahidi: Ilinunuliwa zaidi ya mil 15 lakini haikufika Milioni 20
Wakili: Hukumbuki kwa sababu hukununua wewe si ndio?
Shahidi: Tumenunua kwa pamoja
Wakili: Inakuwaje unasahau bei uliyonunua?
Shahidi: Umepita muda mrefu ndo maana
Wakili: Ulinunua kwa nani ile gari?
Shahidi:Ilikuwa kampuni ya ujenzi
Wakili:Inaitwaje
Shahidi:Sikumbuki lakini ilikuwa kampuni ya ujenzi
Wakili:Mliuziana sehemu gani?
Shahidi:Arusha
Wakili:Arusha sehemu gani Arusha ni kubwa?
Shahidi:Tulikutana kwa Wakili
Wakili:Wakilk gani?
Shahidi:Panaitwa Haraka Law
Wakili:Mwanasheria aliyesaini kwenye hiyo Haraka law alikuwa nani?
Shahidi:Simkumbuki jina
Wakili:Wewe simu unayotumia ni namba ngapi ua kwako nyingine zaidi ya ile nyingine
Shahidi:0754 552520
Wakili:Hii namba uliyotaja ilisajiliwa kwa jina lako wewe?
Shahidi:Mwanzoni ilikuwa imesajiliwa kwa jina langu ila ilipokuja sheria ya kusajili kwa namba ya Nida alinisajilia Lengai kwani sikuwa na namba ya Nida
Wakili:Kwa hiyo kule anasomeka nani?
Shahidi:Itasomeka Lengai
Wakili:Wewe hauna mkopo wowote benki
Shahidi:Ndiyo
Wakili:Sabaya pia hana mkopo
Shahidi:Sifahamu hilo
Wakili:Hufahamu mambo ya mume wako?
Shahidi:Huwezi ukayajua yote
Wakili:Katika kipindi mmeishi umewahi kuona amekopa?
Shahidi:sijui na kusikia sijawahi
Wakili:Unaijua namba ya gari ya serikali aliyokuwa anatumia?
Shahidi:Mi najua ni STK sijawahi ku focus kujua namba
Wakili:Unakubaliana na mimi Sabaya ni mtu maarufu sana
Shahidi:Ndiyo
Wakili:Ni kweli kwamba 22.1.2021 mume wako alivyoondoka asubuhi haujui ni kitu gani alichokifanya huko alipokuwa
Shahidi:Mi najua alienda ofisini
Wakili:Ulikuwa naye ofisini
Shahidi:Sikuwa naye
Akihojiwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tarsila Gervas sehemu ya mahojiano ilikuwa kama ifuatavyo:
Wakili: Jesca kama binti unajua haki zako ni zipi kama mwanamke,mke unazifahamu?
Shahidi:Ndiyo
Wakili:Ni kweli wewe kama mtoto wa kike unayo haki ya kumiliki mali?
Shahidi:Ndiyo
Wakili:Ni ukweli kwamba haki hiyo ni pamoja na mali hizo kuwa kwenye jina lako?
Shahidi:Ndiyo
Wakili:Na ni ukwlei kwamba kati ya mali zote mnamiliki na Sabaya hakuna uliyosema mnamiliki pamoja?
Shahidi:Siyo zote.VX Masai namba T 341 ANT ina jina langu
Wakili:Na Jesca turudi kwEneye hii gari,hii kampuni ya ujenzi iko wapi?
Shahidi:Iko Arusha
Wakili: Na jina la Jesca kwenye hii gari bila shaka TRA ndivyo lilivyo
Shahidi:Ndiyo
Wakili:TRA linasomeka kama nani?
Shahidi: Jesca Thomas
Wakili:Wewe ni wa wapi
Shahidi:Adress yangu ni 61 Usariver
Wakili:Na huu umiliki ulibadilisha lini toka kampuni hii ya ujenzi kuja kwako
Shahidi:Nilibadilisha tu baada ya kununua,2019 mwanzoni
Wakili:Hii 2019 ulikuwa ukiishi wapi?
Shahidi:Bomang'ombe
Wakili:Jana ulisema hufahamu kuhusu minara ya simu?
Shahidi:Ndiyo sifahamu
Wakili:Na bila shaka wakati unaongea na ile namba 0758 707171 ulikuwa unaendesha gari si ndiyo?
Shahidi:Ndiyo
Wakili:Na bila shaka ile siku kulingana na ushahidi wako wa jana uliongea na watu wawili au watatu?
Shahidi:Niliongea na watu wengi
Wakili:Na uliandika meseji ngapi kutumia ile simu?
Shahidi:Sikumbuki ni ngapi
Wakili:Na hii simu uliita ya biashara imesajiliwa kama ya biashara na siyo mtu binafsi
Shahidi:Tulisajili kama mtu binafsi
Wakili: Hii simu ilisajiliwa lini?
Shahidi: 2018 mwishoni
Wakili:Na ni vitu gani vilitumika kusajili
Shahidi:Aliyesajili ni Lengai
Wakili:Hukujua ametumia nini kusajili si ndiyo?
Shahidi:Eeeh
Wakili:Na ni ukweli appartment mliyokamatwa ina stairs kwa juu?
Shahidi:Ilikuwa hotelini ghorofa ila siyo apartment
Wakili:Na ilikuwa Mbezi si ndiyo?
Shahidi:Ndiyo
Wakili:Unafahamu watu wangapi wanaofanya kazi na mume wako
Shahidi: Namfahamu aliyekuwa DAS wake na Mkurugenzi,dereva na mdada alikuwa DMO ndiyo watu walikuwa wanakuja nyumbani
Wakili:Ndugu yako anaishi kwa Morombo anaitwa nani?
Shahidi:Morombo sina ndugu
Wakili: Kwa kuwa kwa mila zao huruhusiwi kuingilia masuala hayo ya kuuza mifugo au namna mume wako anapata hela hela inayokuja hujui imetokana na nini?
Shahidi:Siyo kweli hela inayokuja najua imetokana na kuuza mifugo
Wakili:Akienda kupora
Shahidi:Hajawahi kwenda kupora
Wakili:Turudi kweye mifugo na hujihusishi kwenye mifugo akikuaga anaenda kuuza mifugo na hajauza si kweli huwezi kujua?
Shahidi:Mara nyingi tunafatana
Wakili:Ushuru wa mifugo ile mliyouza Milioni 20,mlilipa kiasi gani?
Shahidi:Inategemea na idadi na bei za ushuru ni kuanzia 1000 hadi 5000 inategemea na mnada ni upi ila sijui kwa sababu mimi sikwenda mnadani
Wakili:Fomu ya maadil ya mume wako ulikaa nayo muda gani kabla ya kupeleka Takukuru kama ulivyosema jana?
Shahidi:Ilijazwa 12/2020.Alikuja nayo ilikuwa ndani
Wakili:Inafananaje hiyo fomu
Shahidi:Ni fomu tu
Wakili:Wewe ulifahamuje ni fomu ya maadili?
Shahidi:Niliambiwa tafuta documebt zote leta ya fomu ya maadili
Wakili:Sasa baada ya kuitafuta umeipata katika kuiangalia inafananaje?
Shahidi:Mimi sikuikagua.Niliambiwa kuna kopi imeandikwa fomu ya maadili
Wakili: Uliyotoa PCCB ni kopi ama origional
Shahidi:Mimi sijui kopi wala origional
Wakili:Labda utukumbushe uliwapa PCCB vitu gani vingine?
Shahidi:Gari VX T 341 ANT,file ya gari namba T 222 BDY ilikuwa na jina la Lengai ndani kulikuwa na mkataba wa mauziano na kadi
Wakili:Hiyo kadi mlipata lini toka TRA?
Shahidi:Sikumbuki
Wakili:Mlinunua lini hilo gari?
Shahidi:Ilikuwa 2020
Wakili:Kingine mlichotoa
Shahidi:Fedha
Wakili:Kiasi gani
Shahidi:Ilikuwa siyo chini ya Milioni 10
Wakili:Mlitoa wapi hizo fedha?
Shahidi: Zilitolewa kwenye akaunti ya biashara
Wakili:Iko benki gani?
Shahidi: CRDB
Wakili:Mlizitoa lini
Shahidi:Sikumbuki lakini tulizitoa tukiwa Dar
Wakili:Kingine?
Shahidi:Simu
Wakili:Ilikuwa simu gani?
Shahidi:Samsung moja ilikuwa Iphone
Wakili:Laini zilizokuwa kwenye hizo simu tuanze na Samsung?
Shahidi: 0758 707171
Wakili: Iphone?
Shahidi: 0754 552520
Wakili:Hii Iphone yenye namba 0754 552520 na wewe ndiyo unatumia?
Shahidi:Ndiyo
Wakili:Unajua majukumu ya mume wako aliyokuwa akiyafanya ya kazi?
Shahidi: Mi najua ni Mkuu wa Wilaya
Wakili:Alikuwa anatakiwa ahakikishe sheria zinafuatwa na yeye pia asivunje aheria na aliapa kufanya hivyo,
Shahidi: Ndio
Wakili:Upendo Wilfred Mbise ni nani?
Shahidi: Simfahamu
Wakili: Jesca Thomas Nassari ni nani
Shahidi: Mimi
Hakimu umesema nani?
Wakili: Upendo Wilfred Mbise mtoto wa mjomba wako hamfahamu
Wakili: Ni kweli Sylvester hujawahi kumuona katika maisha yako?
Shahidi: Simfahamu
Wakili: Kuna mtu ambaye mlikamatwa naye Dar na mlikuwa chumbani yeye alikuw sebuleni humfahamu?
Shahidi: Hapana
Wakili: Unampenda sana mume wako si ndiyo?
Shahidi: Ndiyo
Wakili: Kwanini uliwaambia Takukuru Arusha 4/6/2021 Sabaya ni mchumba wako siyo mume wako?
Shahidi: Niliwahi kuhojiwa mara moja kuhusu Sabaya na ni Dar na nilisema ni mume wangu
Wakili: Hata ulivyokabidhi ulikabidhi kama mchumba na siyo mke na ulikabidhi sakina si ndiyo
Shahidi: Hapana
Wakili: Ninkweli Dar mlikabidhi simu na fedha mbali na gari?
Shahidi: Kila mtu alikuwa anakabidhi za kwake
Wakili: Ulikabidhi simu gani Dar Es Salaam?
Shahidi: Samsung na Iphone
Wakili: Ni kweli kwamba utafanya chochote ili mume wako awe huru
Shahidi: Ambacho hakivunji sheria
Wakili:Wakati mwenzangua nauliza ulisema unaelwqa maana ya kusema uongo mahakamani si ndiyo
Shahidi: Ndio
Wakili: Kuan mchunganmji ulimtaja alifunga ndia yenu ni nani?
Shahidi: Anaitwa Dk Lekundayo
Wakili: Ni wa wapi?
Shahidi: Ni mchungaji na Askofu Arusha Central Churu
Wakili: Tangazo la kwanza la ndoa yenu lilikuwa tarehe ngapi?
Shahidi: Sikumbuki
Wakili: lilitangaza mara ngapi?
Shahidi: Mara tatu
Wakili:Kati yako na mume wako nani muumini wa hilo kanisa?
Shahidi: Yeye na mimi baada ya kufunga ndoa
Wakili: Kabla ya hapo ulikuwa muumini wa kanisa gani?
Shahidi: Lutheran huko Meru
Wakili: Yale maghala yako yako wapi?
Shahidi: Kisongo, Morombo na Tengeru
Wakili: Unanunua wapi hayo mazao?
Shahidi: Nanunua mashambani Loksale, nalima na nanunua Loksale
Wakili: Lengai mara ya kwanza umemuona wapi?
Shahidi: Arusha
Wakili: Mwaka gani?
Shahidi: 2016
Wakili: Udom ulimaliza mwaka gani?
Shahidi: 2016
Wakili wa Serikali Neema Mbwana naye anaanza kumhoji shahidi
Wakili: Shahidi umesema unaishi wapi?
Shahidi: Kwa sasa naishi Sakina
Wakili: Unaishi na nani?
Shahidi: Naishi mwenyewe
Wakili: Huyo mumeo yuko wapi kwa sasa?
Shahidi: Magereza
Wakili: Si mumeo Magereza anafanya nini
Shahidi: Mhehsimiwa nisingependa kujibu hilo swali
Wakili: Nauliza mumeo yuko wapi kwa sasa?
Shahidi: Nikasema magereza
Wakili: Kwanini anaishi Magereza ni mfungwa au mahabusu?
Shahidi: Kama mahabusu kwenye hii kesi
Wakili: Shahidi umesema wewe ni mjasiriamali toka lini?
Shahidi: Toka 2018
Wakili: Imeleta kitu gani umeleta hapa mahakamani kuthibitisha wewe ni mfanyabiasha wa maharage na mahindi?
Shahidi: Sijaleta ikihitajika naleta
Wakili: Shahidi umeshasema uongo mara ngapi hapa mahakamani?
Shahidi: Sijasema uongo
Wakili: Kumbukumbu za biashara yako unaweka wapi?
Shahidi: Inayohitajika nyumbani inakaa nyumbani,inayokaa stoo inakaa stoo
Wakili: Umeleta hapa mahakamani?
Shahidi: Nimesema sijaleta zikihitajika nitaleta
Wakili: Malula unamiliki kiasi gani cha ardhi?
Shahidi: Malula shamba ni kubwa sihawaji kupima
Wakili: Tanga?
Shahidi: eka 11
Wakili: Tanga hizi eka 11 mlinunua kiasi gani?
Shahidi: Na lenyewe nimelikuta
Wakili: Fedha zilizokuwa zinatokana na mauzo ya mifugo zilikuwa zinawekwa wapi?
Shahidi: Nyingine zinawekwa benki CRDB, zingine zinafanyia mambo mengine
Wakili: Hiyo akaunti ni ya biashara au binafsi?
Shahidi:I lifunguliwa kama joint akaunti
Wakili: Mlifungua tawi gani?
Shahidi: Friends Corner
Sasa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekulesehemu ya anamhoji kama shahidi ifuatavyo
Wakili: Umeieleza mahakama kwa nyakati tofauti umekuwa ukiambatana na mume wako akienda kuuza mifugo?
Shahidi: Ndio
Wakili: Kutokana na mila ni sahihi ulikiwa huruhusiwi kujua idadi ya mifugo iliyopo na inayouzwa?
Shahidi: Ni sahihi
Wakili: Ni sahihi ukiwa kama mke halali wa Sabaya hukuwahi kujua mume wako ana mkopo kama ulivyoeleza mahakama?
Shahidi: Ndio
Wakili: Na wala hukujua nyaraka alizotumia Sabaya laini zile mbili ulizokuwa ukitumia kwa biashara na binafsi?
Shahidi: Sikujua
Wakili: Hujui idadi ya kifuhi, hujui iwapo ana mkopo au hana nitakuwa sahihi nikisema wewe kama mke hukujua kila kitu anachokifanya mume wako akiwa mbali na wewe au akiwa anafanya shughuli nyingine?
Shahidi: Nilijua alivyonishirikisha
Wakili: Kwa maana hiyo hata 22.1.2021 ambayo ulidai ulikuwa Arusba huwezi kujua kama yeye na genge lake walikuja Arusha
Shahidi: Nilimwacha Boma
Wakili: Ndoa mlifunga lini
Shahidi: 27.5.2018
Wakili: Ulibatizwa lini?
Shahidi: Nilibatizwa kabla ya ndoa
Wakili: Ulibatizwa sehemu gani
Shahidi: Ikizu, Musoma
Wakili: Umedai hapa leo wewe umebatizwa Ikizu Musoma, mara ya kwanza ulivyoulizwa swali na Tarsila ulisema ulianza kuabudu Sabato baada ya kufunga ndoa
Shahidi: Ndio
Wakili: Ni sahihi ulisema kabla ya ndoa ulianza kuabudu Lutheran kule Meru
Shahidi: Ndiyo
Wakili: Umesema ulibatizwa Ikizu huko ulibatizwa kwa imani ipi?
Shahidi: Nilibatizwa kuingia Sabato
Wakili: Kwanini ulichagua kwenda Ikizu wakati ulisema unakaa Meru?
Shahidi: Sikuamua mimi mwenyewe tulijadiliana na ni sehemu Lengai alibatizwa
Wakili: Jesca nitakuwa sahihi nikisema tangu umeoana na Lengai hujawahi kuwa na maamuzi yako peke yako?
Shahidi: Kitu kama kinanihusu mimi ninayo,kama kinahusu familia tunajadiliana
Wakili: Nitakuwa sahihi nikisema hata wewe kuja kutoa ushahidi hasa kusema Januari 22, 2021 simu ulikuwa nayo wewe ni maelekezo uliyopewa kuja kutoa mbele ya mahakama hii
Shahidi: Ilikuwa maamuzi yangu sijaelekezwa
Baada ya shahidi kumaliza kutoa ushahidi wake Wakili wa utetezi Mosses Mahuna aliielza mahakama kuwa shahidi anayefuata ni mtuhimiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Sabaya ambaye anaanza kujitetea.
Hakimu Patricia Kisinda anasema anaahirisha kesi kwa dakika tano kisha mahakama kurejea, kesi imeahirishwa saa 12:35 mchana.