Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miili sita waliofariki kwa ajali Rombo yatambuliwa

Basi la Ngasere na Noah baada ya kupata ajali katika eneo la Tarakea katika Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Muktasari:

  • Ajali ya basi la Ngasere na Noah iliyotokea katika eneo la Tarakea katika Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro na kusababisha vifo vya watu tisa, miili sita imetambuliwa na ndugu huku mitatu ikiwa bado.

Rombo. Miili sita kati ya tisa ya watu waliofariki kwa ajali ya gari iliyohusisha basi la abiria la Ngasere na Toyota Noah, katika eneo la Tarakea katika Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro imetambuliwa huku mingine mitatu ikiwa bado haijatambuliwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema ajali hiyo imetokea leo Alhamis Desemba 26, 2024, saa 9:40 jioni katika Kijiji cha Kibaoni, Tarakea barabara kuu ya Moshi-Tarakea.

"Leo majira ya saa 9:40 jioni huko Kijiji cha Kibaoni, tarafa ya Tarakea, Wilaya ya Rombo barabara kuu ya Moshi-Tarakea, gari kampuni ya Ngessere ikitokea Dodoma kwenda Tarakea iligongana na gari dogo la abiria likitokea Tarakea kwenda Moshi na kusababisha vifo vya watu tisa waliokuwa kwenye Noah," amesema Kamanda Maigwa.

Kamanda Maigwa amewataja walifariki katika ajali hiyo ni Mamasita Lowasa (27) mkazi wa Kamwanga, Damarisi Kanini Mwikau (22) mkazi wa Elasti Kenya, Peter Urio (38), Monica Mumbua (64) raia wa Kenya, Eligatanasi Kanje (30) mkazi wa Tarakea na Hilda Leberatus (24), mkazi wa Kikelelwa.

Aidha, Kamanda Maigwa, amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Noah akijaribu kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.

Kamanda Maigwa, amesema miili hiyo imehifadhiwa hospitali ya Huruma kusubiri uchunguzi na taratibu nyingine.