Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfanyabiashara wa Tanzanite, kada wa CCM afariki

Mfanyabiashara wa Tanzanite, kada wa CCM afariki

Muktasari:

  • Ni mmiliki wa Hoteli za Gold Crest za jijini Arusha na Mwanza. Alikuwa kamanda wa UVCCM mkoani arusha na mjumbe wa mjumbe wa NEC wa chama. Mwaka 2015 alikuwa kwenye timu ya kampeni ya urais wa Edward Lowassa.

Arusha. Mfanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite, Mathias Manga ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC),  amefariki dunia akitibiwa nchini Afrika Kusini.

Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara, Sadick Mnenei amesema wamepokea taarifa za kifo cha Manga aliyekuwa anayemiliki mgodi wa Tanzanite wa Manga Gems uliopo kitalu D, leo mchana.

"Ni kweli tumepata taarifa za kifo kutoka Kwa watu waliokuwa karibu naye na alikuwa anaumwa hata kupelekwa huko kwa matibabu," amesema.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (Tamida), Sammy Mollel  amesema amepata taarifa za msiba wa Manga.

"Nimepata taarifa lakini wasemaji ni familia, mtafuta mdogo wake nadhani atakuwa na maelezo ya zaidi," amesema Mollel.

Manga pia alikuwa anaendesha Hoteli ya Gold Crest zilizopo jijini Arusha na Mwanza na alikuwa anamikiki majumba kadhaa ya kifahari jijini Arusha.

Mfanyabiashara huyu aliwahi kuwa kamanda wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Arusha na diwani wa Mrangarini wilayani Arumeru.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 alikuwa mmoja wa viongozi wa timu ya kampeni ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ila baada ya uchaguzi huo alivuliwa nafasi zake zote ndani ya CCM. Hata hivyo baadaye alirejeshewa uanachama.