Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge ataka mbolea ipatikane ngazi ya kata

Muktasari:

  • Mbunge wa Mufindi, David Kihenzile amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwekwa utaratibu mzuri wa namna mbolea ya ruzuku inavyoweza kupatikana ngazi ya kata.

Dar es Salaam. Mbunge wa Mufindi, David Kihenzile amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwekwa utaratibu mzuri wa namna mbolea ya ruzuku inavyoweza kupatikana ngazi ya kata.

 Pia ameomba mbolea kuwekwa katika ujazo tofauti ili wakulima wengi waweze kunufaika nayo hata kama wanalima kidogo.

Ametoa maombi hayo leo katika kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane kinachofanyika katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya.

Kihenzile amesema lengo la Serikali kuweka ruzuku ni zuri lakini upatikanaji wa mbolea hiyo huondoa dhana halisi ya mbolea ya rukuzu.

"Mwaka jana kulikuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa mbolea ilibidi ufunge safari hadi makao makuu ya wilaya ili upate mbolea hata ile dhana ya ruzuku ikawa haionekani,"

"Tunaomba kupitia Wizara ya Kilimo, waje na utaratibu mzuri wa namna gani mbolea hiyo iweze kupatikana katika ngazi ya kata ili wananchi hao waweze kunufaika,"

Pia amesema ni vyema kuangalia namna ya mbolea hiyo inavyoweza kupatikana katika ujazo tofauti ili watu wengi waweze kumudu.

"Tunafahamu ukienda mafuta ya kula kuna lita 20, lita10, Lita 5 hadi 1, tunakuomba ikikupendeza, tuanze kutoa mbolea kwenye vifungashio vya kilo tano na kilo moja, ili mtu ambaye ana nusu heka asilazimike kubeba mfuko wa kilo 50,” amesema Kihenzile.

Amesema kufanya hivyo itakuwa ni kuendelea kugusa maisha ya wananchi.