Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Masauni: Watoto wajengwe katika utamaduni wa kuyatunza mazingira yao

Muktasari:

  • Utamaduni wa kutunza mazingira unaanzia katika ngazi ya familia, jamii kisha serikali nayo kwa nafasi yake inatakiwa kuchukua hatua kuhakikisha mazingira yanalindwa.

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandishi Hamad Masauni ametoa wito kwa wazazi kuwajengea watoto utamaduni wa kupenda na kutunza mazingira yanayowazunguka.

Masauni ameyasema hayo alipo shiriki zoezi la usafi wa fukwe ambalo limefanyika chini ya uongozi wa ubalozi wa Saudi Arabia Sanjari na shirika la AHRN na kusisitiza utamaduni wa mtu kuyapenda mazingira yake unaanzia katika ngazi ya familia.

"Utamaduni wa kutunza mazingira unaanzia katika ngazi ya familia, jamii kisha serikali nayo kwa nafasi yake inatakiwa kuchukua hatua kuhakikisha mazingira yanalindwa"

"Wazazi na walezi tuwafunze watoto wetu umuhimu wa kutunza mazingira yanayowazunguka"amesema.

Ameongeza kuwa Serikali itahakikisha inaweka mipango na mikakati ya namna ya kukabiliana na ongezeko la taka hasa mijini kutokana na kasi kubwa ya uzalishaji wa taka hasa katika jiji la Dar es Salaam ambalo linazalisha asilimia 15.3 ya taka zote nchini.

Kwa upande wake Balozi wa nchi ya Saudi Arabia nchini, Yahya Ahmed Okeshi pamoja na mkurugenzi wa shirika la AHRN Olivier Muhizi wamesema nia ya kufanya usafi katika ufukwe za Kawe ni kujenga utamaduni kwa Watanzania kushiriki katika usafi na utunzaji wa fukwe