Masauni ateua wajumbe wa bodi ya TPFCS
Muktasari:
- Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi (TPFCS), limepata wajumbe wapya wa bodi baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni kufanya uteuzi wao ulioanza Julai 28.
Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amefanya uteuzi wa wajumbe tisa wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi (TPFCS).
Waziri Masauni amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 6 (2) (a-g) cha Amri ya Uanzishwaji wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi ya Mwaka 2013, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023.
Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Agosti 3, 2024 na Wizara ya Mambo ya Ndani, imewataja walioteuliwa na Waziri Masauni kuwa ni Omar Issa (mwenyekiti), ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Wengine walioteuliwa ni pamoja na Dk Prosper Kilamuu (katibu), wakati wajumbe ni Dk John Sausi, Selemani Nyakulinga, John Massawe, Moses Luvinga, Nyaswa Machibya, Arafat Ali Haji na Idd Kilima.
“Uteuzi huu umeanza rasmi Julai 28, 2024,”imeeleza taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Ndani.