Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mapinduzi ya kidijitali na jukumu la kuinua wenye ulemavu

Muktasari:

  • Teknolojia ya kidijitali ina jukumu muhimu katika kuwajumuisha watu wenye ulemavu nchini Tanzania. Hata hivyo, changamoto zinazoikabili jamii hii ni nyingi, ikiwemo ukosefu wa ufikiaji wa huduma za mtandao.



Dar es Salaam. Mtandao umekuwa sehemu muhimu ya maisha ya binadamu kwa mawasiliano na huduma mbalimbali kama vile elimu, afya, fedha, usafiri, burudani na biashara.

Tovuti ya Datareportal inakadiria kuwa watu bilioni 5.4, sawa na asilimia 66.2 ya watu wote duniani, wanatumia mtandao mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.8 ya waliotumia mwaka jana. Barani Afrika, takriban asilimia 40 ya watu wako mtandaoni, huku Tanzania, DRC, Msumbiji na Lesotho zikiwa na asilimia 20 pekee ya watu mtandaoni.

Hali hii inaonesha changamoto ya ufikiwaji mtandaoni kwa watu walio pembezoni, hususan watu wenye ulemavu nchini Tanzania. Takwimu zinaonesha kuwa watu wenye ulemavu ni bilioni 1.3 duniani kote, kati yao milioni 45 wakiwa barani Afrika. Nchini Tanzania, kuna watu wenye ulemavu milioni 3.3, wakiwemo wenye ulemavu wa kuona, kusikia, na watumiaji wa viti vya magurudumu.

Vikwazo na dhana nyingi zimekuwa zikiwabagua watu wenye ulemavu licha ya ukweli kwamba wao ni sehemu ya jamii. Doris Mkiva, mwanaharakati wa ulemavu, anasema wanawake walemavu wanakabiliwa na changamoto mara mbili wanakutana na mazingira yasiyo na ufikiaji na mfumo dume.

Washikadau, wakiwemo watetezi wa haki za watu wenye ulemavu, wabunifu wa teknolojia, na watunga sera, walijadili mikakati ya kuunda mazingira jumuishi ya kidijitali katika mjadala uliofanyika jijini Arusha. Mjadala huo, uliokuwa na dhima isemayo "Teknolojia kwa Wote: Kuziba Pengo la Ujumuishi na Ubunifu Kidijitali kwa Watu Wenye Ulemavu," uliangazia changamoto, fursa, na suluhisho za kibunifu.

Mosses Mollel, Mkuu wa Mpango wa Walemavu wa Kituo cha Msaada wa Kisheria cha Ngorongoro, alieleza kuwa anafanya utafiti kuhusu matumizi ya teknolojia ya kidijitali kuwakabili watu wenye ulemavu kufikia huduma za kifedha mtandaoni. Aidha, alisisitiza umuhimu wa mradi wa YODO unaowajengea uwezo vijana wenye ulemavu katika mitandao ya kijamii.

Vodacom Tanzania pia imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma na bidhaa jumuishi kwa watu wenye ulemavu. Doreen Kissoky, Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja, alisema kuwa walibaini changamoto za uelewa wa kuwafikia wateja wenye ulemavu. Vodacom ilianza mpango jumuishi mwaka 2022, ikiwasiliana na watu wenye ulemavu ili kubuni bidhaa zinazokidhi mahitaji yao.

Ingawa kuna juhudi za kuimarisha ujumuishi wa watu wenye ulemavu, bado utekelezaji wa sera na sheria zinazolinda haki zao unakabiliwa na changamoto. Tanzania iliridhia Mkataba wa Kimataifa wa Watu Wenye Ulemavu wa 2006, lakini utekelezaji wa sheria na sera hizi umekuwa dhaifu.

Mjadala huo ulionyesha haja ya kuendelea kuboresha mazingira ya kidijitali ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao za msingi kama watu wengine ifikapo mwaka 2050.