Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama adaiwa kumuua mwanaye kwa kumchapa fimbo

Muktasari:

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, linamshikilia mwanamke mwenye miaka 27, Mkazi wa Kibosho Kirima Juu, Wilaya ya Moshi kwa tuhuma za kumuua mwanae kwa kumchapa na fimbo.

Moshi. Mkazi wa Kibosho Kirima Juu, Wilaya ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro anadaia kumuua mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu na miezi sita, kwa kumchapa kwa fimbo, akimtuhumu kuchezea maji.

 Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27, anadaiwa kufanya mauaji hayo jana Jumapili, Julai 31, 2022, ambapo alimchapa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake.

Inadaiwa alimchapa mtoto huyo akimtuhumu kuchezea maji ya baridi, yaliyokuwa yakitiririka kwenye bomba.

Akizungumza na Mwananchi Digital, leo Jumatatu, Agosti 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (RPC), Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Amesema jina la mwanamke huyo ambaye tayari amekamatwa limehifadhiwa.