Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mali benki ya China zahamishiwa NMB

Muktasari:

BoT imefikia hatua hiyo kwa kutumia sheria ya operesheni zake na hatua hiyo inakuja baada ya NMB kuahidi kuanza kutoa huduma kwa wateja wa benki hiyo ndani ya siku 60.

Dar es Salaam. Benki Kikuu ya Tanzania (BoT) imehamisha mali na madeni yote ya Benki ya Biashara ya China kwenda kwa Benki ya NMB Plc.

BoT imefikia hatua hiyo kwa kutumia sheria ya operesheni zake na hatua hiyo inakuja baada ya NMB kuahidi kuanza kutoa huduma kwa wateja wa benki hiyo ndani ya siku 60.

Gavana wa BoT, Florens Luoga aliwaambia waandishi wa habari kuhusu kuunganishwa kwa benki hizo akisema ni kutokana na kifungu cha 58(1)(g)(i) na (iii) cha Sheria ya benki na taasisi za fedha ya mwaka 2006. Benki hiyo iliwekwa chini ya uangalizi tangu Novemba 19, 2020 ili kuangalia changamoto zinazoikumba.

“Operesheni za kawaida za benki hiyo zilisimamishwa kwa siku 90 ili kuangalia suluhisho jingine,” alisema.

Alisema majukumu ya BoT chini ya kifungu cha 58(4) ya Sheria ya Benki na taasisi za fedha katika mchakato wa kutafuta suluhisho imeonekana mali na madeni yake yahamishwe.

Alisisitiza kuwa wakopaji wa benki hiyo wanatakiwa kulipa mikopo yao kwa mujibu wa masharti na vigezo.

Alisema awali BoT ilikuwa na majadiliano na maofisa wa Benki ya Biashara ya China na viongozi wa benki ya NMB na wakakubaliana kuziunganisha benki hizo.

“Ieleweke Benki ya Biashara ya China haijafilisika kwa kuwa ina mali nyingi, lakini imeshindwa kuendelea na kazi zake na mchakato wake ni mgumu kwa kuangalia kuwa wamiliki wake ni wageni, kwa hiyo tunaiweka chini ya Watanzania kuepusha matatizo yoyote,” alisema.

Alisema mali hizo zitahamishiwa NMB baada ya kufanyika tathmini.

Wakati huo huo, alisema benki za Tanzania hazikuathiriwa na janga la virusi vya corona katika ukanda wa Jangwa la Sahara, badala yake alisema benki nyingi ziliathiriwa na wakopaji wasiorejesha mikopo au wafanyakazi walioathiriwa na corona.

“Kutokana na ukorofi wa wafanyakazi, benki zilijikuta kwenye matatizo ya urejeshaji wa mikopo isiyolipika,” alisema.

Alisema kwa sasa benki zinakabiliana na changamoto ya kujenga mifumo ya mikopo na kuwafikia wananchi kwa lengo la kuboresha kipato.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa NMB Plc, Ruth Zaipuna aliwataka wateja wa Benki ya Biashara ya China wasiwe na wasiwasi kwa kuwa fedha zao ziko salama.

Alisema wateja hao wataanza kupata huduma baada ya siku 60 kutegemea na mfumo wa kutambua wateja utakavyoanza kufanya kazi.

‘Tumeweka matawi yetu likiwemo la Ohio tayari kwa ajili hiyo ikiwa pamoja na kufanya majadiliano na wakopaji,” alisema Zaipuna.