Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majivu ya Mchina aliyeuawa Dar yatakavyozikwa

Muktasari:

  • Mila za Kichina za msiba huhusisha kuchoma mwili wa marehemu na kuhifadhi majivu kwenye kisanduku maalumu, kabla ya kutolewa heshima na kuzikwa kaburini.



Dar es Salaam. Kwa mila na desturi za kichina, mtu anapofariki dunia mwili wake huchomwa moto na majivu yake kuhifadhiwa ndani ya kisanduku maalumu kabla ya kuzikwa kaburini kama ilivyo kwa mazishi ya maeneo mengine.

Baada ya mwili kuchomwa moto, familia hufanya taratibu za mwisho za kuaga majivu, kisha kisanduku hicho huzikwa ardhini kwenye kaburi lililoandaliwa kwa heshima kwa marehemu.

Ni utaratibu huo ambao familia ya mfanyabiashara na mmiliki wa kiwanda cha kuchakata chupa za plastiki cha XIL LI, Bhaozang Ge (50) imeufuata, baada ya mwili wake kuchomwa moto Mei 24, 2026 katika eneo la Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Mmiliki huyo raia wa China aliuawa na watu wanaodaiwa ni walinzi binafsi wa kiwanda hicho kilichopo Mabibo, Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumamosi ya Mei 16, 2026.

Baada ya shughuli ya kuuchoma mwili huo kukamilika, familia majivu ndani ya kisanduku maalumu lililofunikwa kwa kitambaa chekundu tayari kwa safari ya kwenda China kesho Jumatano Mei 27, 2026 kukamilisha maziko.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne, Mei 26, 2026 kwa niaba ya wanafamilia Mhasibu wa kiwanda hicho, Eversophy Michael amesema majivu hayo yatazikwa China kwa kufuata mila za Kichina, ambapo kaburi litachimbwa na kisanduku chenye majivu kufukiwa ardhini kama ilivyo kwa mazishi mengine.

“Waliamua kuuchoma mwili huo hapa nchini badala ya kuusafirisha kwenda China, kwa sababu hata huko bado ungepitishwa katika utaratibu wa kuchomwa moto kabla ya mazishi, hivyo wakaona ni nafuu kubeba majivu pekee,” amesema Eversophy.


Hofu ya wafanyakazi

Mei 24, mwaka huu baada ya shughuli za kuuchoma mwili huo, familia ya Bhaozang Ge iliitisha mkutano na wafanyakazi wa kiwanda ili kuwaondoa hofu iliyokuwa imetanda, kuhusu mustakabali wa ajira zao baada ya kifo cha mwajiri wao.

Katika mkutano huo, mdogo wa marehemu, Baosheng Ge maarufu Denis, mke wa marehemu pamoja na mtoto wake wa kwanza, waliwahakikishia wafanyakazi kuwa shughuli za kiwanda zitaendelea kama kawaida na hakuna mfanyakazi atakayepoteza kazi.

“Mwendelee kufanya kazi kama kawaida, hiki kiwanda kitaendelea kama alivyokuwa na muwe tayari kusukuma kampuni iwe sawa,”alisema Denis mbele ya wafanyakazi hao.

Familia ya mmiliki wa kiwanda cha kuchakata chupa za plastiki cha XIL LI , Bhaozang Ge wakimuaga mpendwa wao kabla ya kupelekwa kuchomwa eneo la Makumbusho jijini Dar es Salaam Mei 24, 2026.

Baadhi ya wafanyakazi walieleza kuwa tangu kutokea mauaji ya Ge Baozhang walikuwa na hofu kubwa kuhusu hatima ya ajira zao, lakini maneno ya familia yamewarudishia matumaini.

Latifa Hussein, mmoja wa wafanyakazi hao amesema eneo hilo ni tegemeo la familia yake hivyo kiwanda kikisimamisha uzalishaji, vijana wengi watakosa kazi na kuhangaika mtaani.

“Hapa ni tegemeo letu ndiyo maana wafanyakazi wamelia kwa uchungu kwa kuondoka bosi wetu, wengine wanawaza wataishije, maana yeye pekee alikuwa tegemeo letu katika maisha ya kila siku,”amesema Latifa.