Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauaji ya Mchina Dar yaiibua Serikali, yatoa tamko

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza katika msiba wa mfanyabiashara na mmiliki wa kiwanda cha kuchakata chupa za plastiki cha XIL LI, kilichopo Mabibo Sokoni, Wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Muktasari:

  • Serikali imesema itaongeza ulinzi kwa wawekezaji kufuatia kuuawa kwa mfanyabiashara na mmiliki wa kiwanda cha kuchakata chupa za plastiki huku shughuli za uchomaji zikifanyika mbele ya wanafamilia wanne pekee.

Dar eSalaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema Serikali imepokea kwa masikitiko kifo cha mfanyabiashara na mmiliki wa kiwanda cha XIL LI, Bhaozang Ge (50), aliyekuwa akichangia maendeleo ya sekta ya uwekezaji na ajira nchini.

Mmiliki huyo raia wa China aliuawa na watu wanaodaiwa ni walinzi binafsi wa kiwanda chake kilichopo Mabibo, jijini Dar es Salaam saa nane usiku wa kuamkia Jumamosi ya Mei 16, 2026.

Amesema Serikali itaendelea kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanakuwa salama kwa wawekezaji wote wanaofanya shughuli zao nchini, ikiwamo kuimarisha masuala ya ulinzi na usalama katika maeneo ya viwanda na biashara.

Amesema tukio hilo linapaswa kuwa somo kwa taasisi na wadau mbalimbali kuhakikisha mifumo ya ulinzi inaongezwa ili kulinda maisha ya watu na mali zao.

Akizungumza leo Jumapili, Mei 24, 2026 katika shughuli ya kuaga mwili wa Bhaozang Ge, Profesa Mkumbo ametoa pole kwa familia ya marehemu, wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania kufuatia msiba huo mzito.

Amesema mchango wa marehemu katika uwekezaji ulikuwa mkubwa kutokana na kuendesha shughuli za uzalishaji zilizosaidia kutoa ajira kwa Watanzania wengi na kuchochea maendeleo ya sekta ya viwanda.

Mtoto wa marehemu Bhaozang Ge akishirikiana na wafanyakazi wa kiwanda cha XIL LI kuutoa  mwili wa baba yake kupelekwa katika eneo la kuchomea lililopo Makumbusho, jijini Dar es Salaam.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, tunatoa pole kwa familia, wafanyakazi wa kiwanda hiki pamoja na ubalozi wa China nchini, huu ni msiba ambao umeigusa Serikali na wadau wa uwekezaji,” amesema Profesa Mkumbo.

Profesa Mkumbo pia amewasihi wafanyakazi wa kiwanda hicho kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu huku akiwasisitiza kuendeleza mshikamano na kazi alizoanzisha marehemu.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Aristides Mbwasi amesema wizara imeguswa na msiba huo na inaungana na familia, ndugu, jamaa pamoja na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

"Serikali itaendelea kuwa karibu na familia katika kipindi hiki huku ikiwaombea faraja na uvumilivu wakati wa maombolezo,"amesema Mbwasi.

Msimamizi wa wafanyakazi wa kiwanda hicho, Lucas Shao amesema kwa kuzingatia utaratibu na mila za familia hiyo, watu watakaoruhusiwa kuingia katika eneo la uchomaji ni wanafamilia wanne pekee, huku waombolezaji wengine wakibaki nje wakisubiri shughuli hiyo kukamilika.

“Tumeambiwa tunaweza kwenda hadi Makumbusho lakini hatutashuhudia shughuli ya uchomaji, kutokana na utamaduni na mila zao, wanaoruhusiwa kuingia kushuhudia ni ndugu wa karibu ambao ni wanne,” amesema Shao.

Amefafanua watakaoingia ndani ni mke wa marehemu, mtoto wake, mdogo wake pamoja na ndugu mwingine wa karibu, huku waombolezaji wengine wakisubiri nje hadi shughuli hiyo itakapomalizika.