Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa ziarani Songwe

Muktasari:

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA), ambako amepokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali kwa ajili ya kuanza ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani humo.

Mbeya. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili leo katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe (SIA) mkoani Mbeya, ambapo atakuwa na ziara ya siku tatu katika wilaya za Ileje na Mbozi mkoani Songwe.

Majaliwa amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma  Homera, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dk Francis Michael , viongozi wengine wa Serikali na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Awali, Dk Michael aliutangazia umma kuwa Waziri Mkuu atafanya ziara ya kikazi kuanzia Novemba 23  hadi 25 mwaka huu katika Wilaya za Ileje na Mbozi ambako atakagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Huu ni muendelezo wa ziara yake aliyofanya Februari 13 hadi 16 katika Wilaya za Momba, Songwe na Tunduma na kesho Novemba 23, 2023 atakuwa Wilaya za Ileje,” amesema.

Amesema Waziri Mkuu atamalizia ziara yake Novemba 24 mwaka huu, katika Wilaya ya Mbozi ambako atatembelea miradi mitatu na kuweka jiwe la msingi katika moja ya miradi hiyo, sambamba na kuzungumza na watumishi na kisha kufanya majumuisho ya ziara yake.

Dk Michael amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya kiongozi huyo sambamba na kushuhudia uzinduzi wa miradi ya maendeleo yenye tija kwa Watanzania na wanasongwe kwa ujumla.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema ujio wa viongozi hao ni fursa kwa wanambeya.