Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yatupilia mbali rufaa zuio mradi wa EACOP

Muktasari:

  • Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ), imekataa kuzuia ujenzi wa mradi bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleani (Tanga), ikisema maombi hayo yaliletwa nje ya wakati na hivyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo.

Dar es Salaam. Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ), imetupilia mbali rufaa iliyokuwa inalenga kusitishwa kwa ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), wenye thamani ya dola bilioni nne.

Bomba hilo lenye urefu wa kilomita 1,443; litasafirisha mafuta ghafi kutoka Ziwa Albert Kaskazini Magharibi mwa Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Mtandao wa RFI umeripoti kuwa uamuzi huo ulitolewa Jumatano, Novemba 29, 2023 ambapo EACJ ilisema kuwa kesi hiyo ya kupinga mradi huo, iliwasilishwa kwa kuchelewa kwa hivyo ilikuwa imepitwa na muda na haikuwa na uwezo wa kuisikiliza.

Mradi huo ambao unajengwa na Serikali za Uganda na Tanzania kwa ushirikiano wa kampuni ya mafuta ya TotalEnergies na kampuni ya mafuta ya China (CNOOC) umekuwa ukipingwa na jamii na watetezi wa mazingira.

Shirika la Natural Justice na mashirika likishirikiana na mengine matatu ya kiraia yanayojishughulisha na uhifadhi wa mazingira, yalifungua kesi hiyo mwaka 2020, yakidai mradi unawaondoa kwa nguvu katika makazi yao, raia ambao bomba hilo litapita katika maeneo yao.

Sambamba na hilo, Watetezi hao wa mazingira, walidai kuwa mradi huo unafukua makaburi ya watu waliyozikwa kwenye maeneo ambayo bomba litapita, lakini pia mradi utaleta athari kwenye mazingira.

Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo, Natural Justice na washiriki wenza katika kesi hiyo, wamesema watakata rufaa ya uamuzi huo.

Taarifa kutoka EACOP zinaonyesha kuwa tayari iliishafikia makubaliano ya awali na Serikali za Tanzania na Uganda katika makubaliano ya Serikali mwenyeji na mradi huo, hatua ambayo inaelezwa kuwa ni ya msingi kuelekea utekelezaji wa mradi huo.

Inaelezwa kuwa bomba hilo la mafuta ghafi, litafungua fursa Afrika Mashariki kwa kuvutia wawekezaji, na kwamba litasababisha kuwepo kwa ongezeko la zaidi ya asilimia 60, ya fedha za moja kwa moja za Kigeni (FDI) nchini Uganda na Tanzania katika kipindi cha ujenzi.