Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yaionya Serikali kesi ya bosi Jatu PLC

Muktasari:

  • Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitaka Jamhuri kuhakikisha inakamilisha upelelezi katika kesi ya utaka ya Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jatu PLC, Peter Gasaya iliyoahirishwa hadi Agosti 28, 2023.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa Jamuhuri katika kesi inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jatu PLC, Peter Gasaya kuhakikisha shauri hilo linapokuja tarehe ijayo wawe na maelezo sahihi ya kujua upelelezi umefikia hatua gani.

Akizungumza leo Agosti 14, Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate amesema upande wa mashtaka wanapokuja mahakamani tarehe ijayo wahakikishe wanakuja na maelezo yaliyo sahihi ya hatua ya upelelezi umefikia wapi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali Frenky Michael kuieleza mahakama hiyo kuwa kesi ilikuja kwa ya kutajwa lakini upelelezi bado haujakamilika.

"Mshtakiwa aliandika barua ya kuomba kukiri makosa yanayomkabili na yeye mwenyewe aliomba kujiondoa kwenye mchakato huo wakati huo kesi haikuweza kuendelea hivyo tunaiomba mahakama hii itupe muda ili wafuatilie upelelezi umefikia hatua gani," alidai Michael.

Hata hivyo, wakili wa utetezi Mafikile Mwamboma aliyeukosoa upande wa mashtaka, akisema shauri hilo awali lilikuwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio na upelelezi wake ulikuwa umekamilika na hatua iliyofika ya kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa huyo.

Mwamboma amedai shauri hilo liliondolewa na mshtakiwa huyo alisomewa upya mashtaka hayo hayo kwa Hakimu Kabate ambapo sheria ya mwenendo wa jinai inasema kesi ikifutwa na kufunguliwa upya inatakiwa upelelezi uwe umekamilika.

"Tunaiomba mahakama hii itupe maelekezo ya sababu ya upande wa Jamuhuri kuendelea kusema upelelezi bado haujakamilika wakati siyo sahihi," amesema Mwamboma.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Agosti 28, 2023 kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa ameendelea kukaa rumande kwa kuwa shtaka lake halina dhamana.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kati ya Januari Mosi, 2020 na Desemba 31, 2021 katika Jiji la Dar es Salaam, akiwa kama Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, kwa njia ya udanganyifu alijipatia zaidi ya Sh5.1 bilioni kutoka  Saccos ya Jatu.