Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maandamano ya Chadema Mwanza mguu sawa

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu akiongoza msafara wa maandamano ya wananchi na wafuasi wa chama hicho kwenye maandamano ya amani yaliyoanzia Buhongwa kwenda uwanja wa Furahisha jijini humo. Picha na Mgongo Kaitira

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe leo Februari 15, 2024 amewaongoza wafuasi na wapenzi wa chama hicho katika maandamano yanayofanyika katika maeneo ya Buhongwa, Igoma na Ilemela Kanisani jijini Mwanza.

Mwanza. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe leo Februari 15, 2024 amewaongoza wafuasi na wapenzi wa chama hicho katika maandamano yanayofanyika katika maeneo ya Buhongwa, Igoma na Ilemela Kanisani jijini Mwanza.

Viongozi wengine walioambatana naye ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar wa chama hicho, Salum Mwalimu, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), John Pambalu na mwanaharakati wa Sauti ya Watanzania, Dk Wilbrod Slaa.

Wengine wanaotarajiwa kushiriki maandamano hayo yatakayofanyika kwenye njia kuu tatu na kumalizikia kwa mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha ni Wakili Boniface Mwabukusi, Mwanaharakati Mdude  Nyagali , Wajumbe wa Kamati kuu ya Chadema, wabunge wa zamani na viongozi wa chama hicho kutoka maeneo tofauti nchini.

Licha ya licha ya mvua iliyoanza kunyesha kuanzia saa 12 alfajiri wanachama na wafuasi wa Chadema wamejitokeza kwa wingi katika maandamano hayo.  

Maandamano hayo ambayo ni ya pili kufanyika baada ya yale ya Dar es Salaam ya Januari 24, 2024 yameitishwa na chama hicho kwa lengo la kumtaka Rais Samia Suluhu Hassan kutosaini miswada ya Sheria za Uchaguzi zilizopitishwa na Bunge wiki zilizopita.

Pia Chadema wanaandamana wakiitaka Serikali kuingilia kati na kushusha gharama za maisha zinazotokana na mfumuko wa bei kwenye bidhaa muhimu.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na chama hicho, baada ya Mwanza maandamano mengine yanatarajiwa kufanyika katika Jiji la Arusha na Mbeya.

Wanavyosema waandamanaji

Akizungumza eneo la Gadh hall ambapo waandamanaji wa njia zote watakutana, Justina Samweli amesema licha ya mvua kunyesha amefika saa 2 asubuhi hii kuwapokea wengine wanaoungana nao kwaajili ya kuelekea uwanja wa Furahisha.

“Mvua ya leo ilikuwa Baraka…kama alivyosema jana Dk Slaa inyeshe mvua, liwake jua tutaandamana na kweli japo bado watu wachache hapa lakini tumejitokeza kuwapokea wenzetu,” amesema

Muandamanaji mwingine katika njia ya Buhongwa ambaye ni mkazi Kata ya Nkinga Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Felister Andrea amesema anaandamana ili kupata Katiba Mpya itakayotoa kipaumbele kwa wananchi na kuhamasisha usikilizwaji wa maoni yao.

"Tukiwa na Katiba Mpya na Tume Huru ya uchaguzi kwa sababu tukiwa na vitu hivyo ni rahisi hata kupata viongozi wanaotusikiliza," amesema Felister.

Naye mkazi wa Kata ya Bukindo Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwnza, Bandio Lukantanga ametaja sababu ya ugumu wa maisha kuwa imemsukuma kuungana na Chadema kufanya maandamano ili kufikisha kilio cha ugumu wa maisha kwa mamlaka husika.

Mwandamanaji wa njia ya Ilemela Kanisani ambaye pia ni mkazi Kabuhoro Kirumba jijini Mwanza, Emmanuel Mtani (81) amesema licha ya uzee wake, ugumu wa maisha ndiyo umemfanya ajiunge kwenye maandamano hayo akiiomba Serikali kama imeshindwa kutatua changamoto za maisha zinazowakabili wananchi basi iachie madaraka.

“Nimefika hapa saa 1:15 asubuhi na kilichonifanya nije ni ukombozi wa Wananchi. Naamini kupitia maandamano haya tutapeleka ujumbe ambao Serikali hii inaweza ikautii,” amesema Jovin Mangu mwandamanaji njia ya Ilemela Kanisani.