Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lowassa alazwa Muhimbili

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa

Muktasari:

  • Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.

  

Arusha. Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo.

Taarifa kutoka kwa familia hiyo zinasema kuwa kiongozi huyo amelazwa katika hospitali hiyo kwa karibu wiki nzima baada ya kufanyiwa upasuaji.

Akizungumza leo Ijumaa Januari 28, 2022 na Mwananchi, Mbunge wa jimbo la Monduli, Fredrick Lowassa ambaye ni mtoto wa Lowassa amesema baba yake alilazwa katika hospitali hiyo alipopatwa matatizo ya tumbo.

"Baba alilazwa kama siku tano zilizopita. Wala haina siri, alifanyiwa upasuaji wa tumbo, lakini bahati mbaya ikaleta complication (hitilafu). Alifanyiwa hapo hapo Muhimbili,” amesema Fredrick.

Amesema wanaomba watanzania, kuendelea kumuombea ili afya yake iendelee kuimarika

"Tunashukuru sana kwa maombi ya Watanzania na tuna imani ataruhusiwa kurejea nyumbani," amesema.