Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lissu asema uchaguzi Chadema ukiwa na mizengwe asitokee wa kumnyamazisha

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Picha na Maktaba

Muktasari:

  • Lissu amesema wanachokitaka wanachama ni uchaguzi ulio huru na haki na hapo akishindwa hatakuwa na la kusema.

Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu amesema endapo uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho utakuwa huru na wa haki na ikitokea ameshindwa atakubali, lakini akishindwa katika mazingira aliyoita ya mizengwe, asitokee mtu wa kumnyamazisha.

Ameyasema hayo leo Desemba 12 alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kutangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho jijini Dar es Salaam.

Lissu amesema alijiunga na chama hicho bila kuwa na chama chochote na kwamba yeye ni mwanamageuzi bila kujali cheo.

“Leo hapa nilipo sio mwenyekiti, maana yake itakuwa sijawa mwenyekiti, nitaacha kuwa Tundu Lissu kwa sababu sio mwenyekiti? Huu umakamu mwenyekiti niliupata nikiwa kitandani? Mimi ni mwanamageuzi na maisha yangu yote nitakuwa mwanamageuzi,” amesema.

Hata hivyo, amesema kinachotakiwa na wanachama ni uchaguzi huo kuwa huru na wa haki. “Wanachokitaka wanachama ni uchaguzi ulio huru na haki, kukiwa na uhuru nitakuwa na cha kusema? Kukiwa na mizengwe kutakuwa na mtu wa kusema ninyamaze?” amehoji.

Ameongeza, “Bahati nzuri nina mdomo mpana na ninautumia vizuri.”

Awali akizungumzia mfumo wa uchaguzi unaoendelea ndani ya chama hicho, Lissu amesema kwa yaliyotokea kwenye uchaguzi huo yamethiubitisha una shida.

“Kuhusu mfumo wetu wa uchaguzi, tunapataje nguvu ya kunyoosha vidole kwa watawala wa nchi hii kama sisi hatuko hivyo? Mimi ni Mkristo, kuna mahali pameeandikwa, toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo uone kibanzi kwenye jicho la mwenzako. Tunahitaǰi chaguzi huru na za haki kwenye chaguzi zetu. Ili tupate moral authority (uhalali) ya kusema, tunataka tume huru, lazima tuwe na uhuru kwenye chaguzi zetu,” amesema Lissu.


Kwanini hajafanyia mkutano makao makuu ya Chadema?

Lissu aliyefanyia mkutano wake katika ukumbi wa Mlimani City jijini hapa, amesema ametumia eneo hilo ili kuwa huru kutokana na minyukano ya uchaguzi inayoendelea.

"Kwa jinsi minyukano ilivyo katika mitandao ya jamii na tension hii, ingeweza kuleta sintofahamu. Tumekuja huku ili niweze kuzungumza nanyi bila hofu.

“Miezi michache iliyopita, kuna bwana mmoja alitangaza kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti, alitangazia kwenye hoteli pamoja na kwamba yeye ni mwenyekiti wa kanda ya Victoria,” amesema.

Mwenyekiti wa Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje ndiye aliyetangaza kugombea nafasi ya umakamu mwenyekiti wa chama hicho.