Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lindi kutangaza fursa za uwekezaji, madini

Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Zuwena Jiri akizungumzia maonyesho ya madini na fursa za uwekezaji zitakazofanyika wilayani Ruangwa Agosti 21 hadi 26. Picha na Joseph Lyimo

Muktasari:

  • Mkoa wa Lindi unatarajia kufanya maonyesho ya madini, kilimo, mifugo, misitu na fursa za uwekezaji Agosti 21 hadi Agosti 26 mwaka 2023.

Lindi. Mkoa wa Lindi unatarajia kufanya maonyesho ya madini na fursa za uwekezaji yatakayohusisha wafanyabiashara na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Mkoa wa Lindi yanapatikana na kuchimbwa madini ya aina mbalimbali ikiwemo dhahabu, nikeli, ganeti ya kijani, manganese ore, marble, jasi na ulanga (kinywe).

Katibu Tawala wa mkoa wa Lindi, Zuwena Omary Jiri akizungumza na Mwananchi Digital jana Jumatano Agosti 17 amesema maonyesho hayo yatafanyika kwa muda wa siku sita wilayani Ruangwa Agosti 21 hadi 26.

Jiri amesema tamasha na maonyesho hayo yatahusisha fursa mbalimbali zinazopatikana mkoani Lindi ikiwemo madini, utalii, kilimo, mifugo na uvuvi.

"Lengo ni kuangazia fursa zilizopo mkoani Lindi na kujenga jukwaa ambalo wadau wa sekta ya madini na sekta shirikishi watapata nafasi ya kujadiliana, kubadilishana uzoefu na kutangaza fursa zilizopo mkoani Lindi," amesema Jiri.

Amesema wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwemo wafanyabiashara, wawekezaji na wapenda maendeleo tofauti kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki tamasha na maonyesho hayo.

Amesema kauli mbiu ya maonyesho hayo ni wekeza Lindi kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya jamii.