Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

LHRC yabaini mapengo rasimu sera ya elimu

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • LHRC yafanyia uchambuzi rasimu ya sera ya elimu ikieleza maeneo ambayo hayajaguswa kwenye sera hiyo licha ya umuhimu wake.

Dar es Salaam. Siku chache baada ya Serikali kuweka hadharani rasimu ya sera ya elimu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeeleza kuwa bado kuna mambo muhimu ambayo hayajazingatiwa.

Mojawapo ya mambo hayo ni sera kutowatambua maofisa elimu utamaduni, maofisa elimu taaluma, maofisa elimu sekondari na maofisa elimu tehama.

Akizungumza leo Mei 11 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga amesema licha ya maofisa hao kuwepo kwenye mfumo elimu nchini, rasimu ya sera haijazungumzia chochote kuhusu watendaji hao.

Kufuatia hilo LHRC imependekeza nafasi hizo zitambuliwe kwenye sera au zifutwe kama hazipo kwenye muundo wa kiutawala.

Mbali na hilo Anna ameeleza kuwa rasimu ya sera haijagusia suala la wasichana waliopata ujauzito wakiwa shuleni kuruhusiwa kurudi shuleni baada ya kujifungua.

“Serikali imeruhusu wanafunzi wanaoacha shule kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito kupata nafasi ya kurudi shule baada ya kujifungua, rasimu ya sera ya elimu haionyeshi hilo, hii inatupa wasiwasi,” amesema Anna.

Jambo lingine ambalo ameeleza kuwa halijawekwa vizuri ni adhabu ya viboko kwa wanafunzi hasa katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na matukio ya wanafunzi kupigwa hadi kupata majereha au kupoteza maisha.

“Kwenye rasimu suala la adhabu shuleni halijazungumziwa kabisa, tunaona umuhimu kwa hili kutokana na matukio ambayo yamekuwa yakitokea. Serikali ieleze wazi je viboko vitaendelea kuwepo?” amehoji Anna.

Hata hivyo Mei 9 mwaka huu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda alitangaza kufungua milango kwa wadau kutoa maoni kuhusu sera hiyo huku akibaibisha kuwepo kwa kongamano la siku tatu kuanzia Mei 12 had