Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lema kuanika ushahidi wa madiwani waliojiuzulu

Muktasari:

Nassari amesema wana ushahidi wa kielektroniki kuhusu tuhuma walizotoa.

Dar es Salaam. Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema kesho Jumapili ataweka hadharani ushahidi wa tuhuma walizonazo kuhusu madiwani wa chama hicho waliojiuzulu wakisema ni kutokana na kuunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli.

Lema na mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari wamewatuhumu madiwani hao wakisema uamuzi wao unatokana na rushwa.

Hata hivyo, madiwani hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikanusha tuhuma hizo.

Lema akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi, amesema wataweka hadharani ushahidi huo kesho kabla ya Jumatatu kuupeleka kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).