Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa siku 10 kuanzia leo, hali ya hewa itakuwa hivi

Muktasari:

  • Kutakuwa na vipindi vya mvua zinazoambatana na ngurumo za radi katika baadhi ya maeneo.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa mwelekeo wa hali ya hewa kwa siku 10 kuanzia leo Jumapili, Juni 1, 2025, ikieleza uwepo wa mvua zinazoambatana na ngurumo za radi zinatarajiwa kunyesha baadhi ya maeneo ya nchi.

Mvua hizo zinatarajiwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria, ikiwemo Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara.

Taarifa ya mwelekeo wa hali ya hewa kwa siku 10 iliyotolewa leo Juni 1, 2025 na TMA kupitia tovuti yake rasmi imeeleza hali itakavyokuwa kwa kila mkoa.

Kwa mikoa ya nyanda za juu kaskazini mashariki, inayojumuisha Arusha, Manyara na Kilimanjaro kutakuwa na vipindi vya mvua nyepesi kwa maeneo machache.

"Pwani ya kaskazini ikijumuisha mikoa ya Tanga, kaskazini mwa Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, itashuhudia vipindi vya upepo mkali na mvua katika maeneo machache," imeeleza taarifa hiyo.

Kwa upande wa mikoa ya magharibi, ikiwemo Kigoma, Katavi na Tabora, vipindi vya mvua vinavyoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache.

Kwa kanda ya Kati inayojumuisha Dodoma na Singida, hali ya ukavu inatarajiwa kuendelea huku nyanda za juu kusini-Magharibi Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa kumeelezwa kutakuwa na hali ya ukavu kwa ujumla.

"Pwani ya kusini, inayojumuisha mikoa ya Mtwara na Lindi, inatarajiwa kupata vipindi vya upepo mkali na mvua katika baadhi ya maeneo, Kanda ya Kusini, ikiwemo Ruvuma na kusini mwa Morogoro, hali ya ukavu inatarajiwa kuendelea," taarifa hiyo imeeleza.

Hali itakavyokuwa usiku

Kuanzia saa 3:00 usiku wa leo Jumapili, TMA imeeleza kutakuwa na mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera na Mara, huku vipindi vya jua vikishuhudiwa.

Aidha, mikoa ya Lindi, Mtwara, visiwa vya Unguja na Pemba, Dar es Salaam, Tanga na Pwani itakuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

"Mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Morogoro, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma, Katavi, Ruvuma, Songwe, Rukwa, Songea na Mbeya inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua," imeeleza TMA.

Kwa mujibu wa TMA, upepo wa pwani unatarajiwa kuvuma kutoka kusini kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa katika pwani yote, huku hali ya bahari ikitarajiwa kuwa na mawingu kiasi.