Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwa nini Samia anaenda India?

Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi katika mwendelezo wa ziara yake katika mkoani Lindi.

Muktasari:

  • Ingawa biashara baina ya Tanzania na wafanyabiashara kutoka bara Hindi ina historia ya karne nyingi zilizopita na uhusiano rasmi wa kiserikali ukiwa umedumu kwa zaidi ya miaka 50, ziara hii ni ina ladha tofauti.

Dar es Salaam. Kesho Jumapili Oktoba 8 Rais Samia Suluhu Hassan anaanza rasmi ziara ya siku tatu nchini India, ambapo Tanzania inatarajiwa kunufaika katika sekta mbalimbali ikiwemo za afya na kilimo.

Ziara ya kitaifa ya Rais Samia nchini India imekuja wakati mwafaka katika kipindi hiki ambapo mataifa haya mawili yanahitajiana katika kiuchumi, kijamii na kiteknolojia.

Ingawa biashara baina ya Tanzania na wafanyabiashara kutoka bara Hindi ina historia ya karne nyingi zilizopita na uhusiano rasmi wa kiserikali ukiwa umedumu kwa zaidi ya miaka 50, ziara hii ni ina ladha tofauti.

Taifa la India liko njiani kuzipiku Japan na Ujerumani na kuwa taifa la tatu kwa uchumi duniani nyuma ya Marekani na China na linahitaji malighafi zaidi kukuza uchumi wake zaidi.

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Kiafrika zenye uchumi unaokua lakini kutoka kuwa nchi masikini hadi ule wa kati na tajiri, inahitaji mitaji, uwekezaji mkubwa na soko la kuuzia malighafi zake duniani.

India inahitaji malighafi na mazao ikiwemo mbaazi na korosho kutoka Tanzania ili kulisha watu wake wanaokisiwa kufikia bilioni 1.3.

 Tanzania inahitaji kutumia mitaji kutoka kwa matajiri wa India na utaalamu wa teknolojia na biashara zaidi ili kukuza uchumi wake.

Vitu vichache katika ziara hii vinaonyesha namna ziara hii ya Rais Samia ya kwanza kufanywa na Rais wa Tanzania nchini India katika muda wa miaka minane, itakavyokuwa tofauti na za miaka iliyopita.

Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba aliwaambia wanahabari kuwa ujumbe wa wafanyabiashara takribani 80 wa Tanzania utafuatana na Rais Samia katika safari yake hiyo.

Wafanyabiashara hao wanatoka katika maeneo ambayo ama yanatafuta fursa na masoko zaidi au yanayohitaji mitaji zaidi na ushirikiano kutoka India ili yapige hatua.

Kwa mujibu wa Waziri  Makamba, Serikali tayari imetenga eneo la ekari zaidi ya 1,000 nchini Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa viwanda kutoka India ili kukuza uwezo wa uzalishaji wa Taifa na  kuongeza ajira kwa Watanzania.

Eneo lingine linalopewa umuhimu wa kipekee kwenye ziara hii ni suala la afya. India kwa sasa ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa uzalishaji wa dawa na matumizi ya teknolojia ya kisasa kwenye matibabu.

Rais Samia amewahi kuzungumza hadharani kwamba anaguswa sana na changamoto za kiafya zinazowakabili Watanzania na ziara hii inajibu mojawapo ya changamoto hizo.

Lakini katika mkutano wake wa juzi Waziri Makamba alisema Rais Samia atasaini makubaliano ya uwekezaji wa taasis ya utoaji wa huduma za kupandikiza figo hapa nchini.

Tatizo la figo ni miongoni mwa matatizo yanayoongezeka hapa nchini yakiathiri watu wengi. Matibabu yake ni gharama kubwa na wenye uhitaji wa huduma hiyo huonekana kama wana hukumu ya kifo.

Mwananchi limezungumza na mtaalamu wa masuala ya figo, Dk Shija Kessy kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma aliyesema uwepo wa taasisi itasaida Tanzania kuwa na miundombinu itakayoweza kukabiliana na changamoto hiyo.

“Taasisi itakayoanzishwa haitajikita kutibu ugonjwa bali itaongeza elimu kwa wananchi ya namna ya kujikinga magonjwa yanayosababisha figo kushindwa kufanya kazi. Matokea yake kutakuwa na watalaamu wanaojua tatizo la figo kwa ukubwa.

 “Itasaidia kuvutia wagonjwa kutoka mataifa ya jirani kuja Tanzania kupata matibabu na kuwezesha Tanzania kupata fedha za kigeni. Gharama ya kupandikiza figo ni kati ya Sh 32 milioni hadi Sh 40 kwa mtu mmoja kupandikwa, uchunguzi na kulazwa kwa mwezi mzima,” amesema Dk Kessy.

Machi mwaka 2022 aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Alfelo Sichwale alisema Watanzania 5,800 hadi wanahitaji huduma ya kusafisha damu au kupandikizwa figo.

Lakini kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha kwa kila watu 10, mtu mmoja mfumo wa utendaji kazi wake figo zake hauko vizuri.

Hii ni sawa na makadirio ya asilimia 10 kwa wananchi wote kusumbuliwa na tatizo hilo, huku asilimia 2.4 wakipoteza maisha na asilimia 2.7 wakigundulika kwenye hatua ya mwisho

Kwenye ziara hiyo ya kihistoria, Rais Samia anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo ya faragha na baadaye mkutano na waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi.

Pia, atakutana na kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya India Droupadi Murm Oktoba 9 mwaka huu.Ziara hiyo Rais Samia  inatarajiwa kukamilia Oktoba 11.