Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumbe mahausigeli wengine hudanganywa hivi!

Muktasari:

Wafanyakazi hao walidai kuwa hawapewi mikataba ya kazi, hawathaminiwi na hukumbana na mateso ya kila aina.

Mwanza. Baadhi ya wafanyakazi za ndani wamedai hurubuniwa kupelekwa mijini kwa ajili ya kusomeshwa, badala yake hujikuta wakigeuzwa kuwa ‘mahausigeli’.

 Wakizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto jijini Mwanza, walisema hawapewi mikataba ya kazi, hawathaminiwi na hukumbana na mateso ya kila aina.

 Veronica Marko na Agness Benedicto, walisema walitolewa vijijini kwa kisingizio cha kusomeshwa, badala yake wanafanyishwa kazi za nyumbani kwa mateso na manyayaso.

 “Watoto wengi tunatolewa vijijini kwa ahadi za kuja kusaidiwa lakini tunapofika mijini tunaingizwa kufanya kazi za nyumbani na wakati mwingine bila ujira,” alisema Agness.

 Ofisa Sheria wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto Wafanyao Kazi za Nyumbani (WoteSawa), Jackline Ngalo alisema utafiti unaonyesha asilimia 80 ya watoto wanaofanya kazi za nyumbani husababishwa na umaskini wa kipato.