Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kortini kwa kujifanya ofisa wa Takukuru

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Mfanyabiashara Edson Beyanga (40), Mkazi wa Bunju A, jijini Dar es salaam, amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kujifanya ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). 

Dar es Salaaam. Mfanyabiashara Edson Beyanga (40), Mkazi wa Bunju A, jijini Dar es salaam, amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kujifanya ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). 

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Gloria Mweinyekule; mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amiri Msumi, amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka ya kujifanya ofisa, wa Takukuru pamoja na kutengeneza nyaraka za kugushi.

Mweinyekule amedai kuwa kati ya Disemba 11, 2020 na Disemba 15, 2020 maeneo ya jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alijifanya ofisa wa Takukuru anayejulikana kama Juma Tambwe.

Alidai kuwa kati ya Agosti 4, 2018 katika jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa aligushi nyaraka ambayo ni kadi ya kitambulisho cha mfanyakazi yenye jina la Boniface Mrema, kama kitambulisho halisi kilichotengenezwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc).

"Upelelezi umekamilika naiomba mahakama hii ipanga tarehe ya kuanza kasikiliza ushahidi na vielelelezo," amedai Mweinyekule.

Kwa mujibu wa wakili huyo wa Serikali, upande wao utanatarajia kuwa na mashahidi na vielelezo kwa ajili ya usikilizwali

Hakimu Msumi amesema dhamana ipo wazi hivyo mshtakiwa huyo anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh1 milioni.

Hata hivyo mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti hayo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 12, 2023.