Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kizimbani akidaiwa kusafirisha mirungi kilo 5.46

Muktasari:

  • Mshtakiwa Mariam Makesa (54), Mkazi wa Sahara Nzingari, jijini Tanga; alikamatwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kutoka moshi kwenda Dar es salaam, zenye uzito wa kilo 5.46.

Dar es Salaam. Mkazi wa Sahara Nzingari, jijini Tanga, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi, kutoka Moshi kwenda Dar es Salaam, zikiwa na uzito wa kilo 5.46.

 Hati ya shtaka hilo ambayo imesomwa na Wakili wa Serikali, Erick Kamala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio, wakili huyo amedai kuwa Mei 19, 2023; maeneo ya Makanya wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro, mshtakiwa alikamatwa akisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi yenye uzito wa kilo 5.46.

Baada ya kusomewa shtaka linalomkabili mshtakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo.

Kamala amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, na kwamba wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa huyo.

Kwa upande wake Hakimu Mrio, ametoa masharti ya dhamana akisema kwamba mshtakiwa huyo anatakiwa awe na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh5 milioni na wawe na vitambulisho halali vya uraia.

Hakimu Mrio ameahirisha kesi hiyo hadi Octoba 2, 2023 na mshitakiwa amerudishwa mahabusu kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana hiyo.