Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiwanda cha kuchakata samaki kujengwa Tanga

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akishika mojawapo ya  samaki waliokabidhiwa na kampuni ya uvuvi ya Albacora

Muktasari:

  • Serikali ya Tanznaia na kampuni ya uvuvi ya Albacora wamekubaliana kujenga kiwanda cha kuchakata mazao ya samaki mkoani Tanga.

Dar es Salaam. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kampuni ya kimatifa ya uvuvi ya Albacora, imekubali kuanzisha kiwanda cha kuchakata samaki kitakachoajiri Watanzania takribani 100.

Ulega ameeleza hayo  jana, Novemba 23, 2023 wakati akipokea samaki tani 50 kutoka katika meli ya Albacora katika Bandari ya Dar es Salaam, ambao watapelekwa katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri.

Albacora ni kampuni ya Uhispania, inayofanya uvuvi kwenye bahari kuu, ina meli kubwa ya uvuvi wa samaki na kiwanda cha kuchakata mazao ya samaki nchini humo.

Waziri Ulega amesema Albacora wamekuwa na utaratibu kuwa baada ya kuvua samaki aina ya jodari wanawasafirisha hadi Hispania kwa ajili ya uchakataji, lakini kutokana na ushawishi wa Serikali wamekubali kuanzisha kiwanda nchini ili shughuli hizo zifanyike hapa.

“Wamekubali na hivi tunavyozungumza wameshanunua ardhi mkoani Tanga kwa ajili ya kuweka kiwanda. Hii meli ina mabahari wengi miongoni mwao ni vijana wa Kitanzania wanaoendelea kupata uzoefu.

“Jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuanzisha bandari ya uvuvi Kilwa (Lindi), zitawezesha meli kama hii kutia nanga huko na nyingine tutaijenga Bagamoyo mkoani Pwani. Tutafungua milango katika sekta ya uvuvi, meli aina hii haziji kwa wingi kwa sababu eneo hili (bandarini) si maalumu kwa meli za samaki,” amesema.

Kuhusu meli hiyo, Waziri Ulega amesema ina urefu wa mita zaidi ya 100 kwa ajili ya kuvua samaki katika maji ya kina kirefu baada ya kupewa leseni na Serikali ya Tanzania.

Waziri Ulega amesema leseni waliopewa Albacora ni maalumu kwa ajili kuvua samaki aina ya jodari, ikitokea wamepata samaki tofauti wanapaswa kuwarudisha serikalini.

“Hata hivyo, kampuni hii imekuwa waugwana kila wanapopata samaki tofauti wanarudisha kwa Serikali na huuzwa katika mnada kwa wahitaji wa bei ya chini,” amesema Ulega.

Mwalikishi wa Albacora, Juven Erekaixn amesema wanajisikia faraja kufikia hatua hiyo na kiwanda kitajengwa haraka iwezekanavyo baada ya taratibu zote kukamilika.

“Tumeshanunua ardhi, sasa wakati wowote tutaanza ujenzi, tunamaliza taratibu ndogo ndogo, tunajisikia faraja kutokana na ukarimu ulionyeshwa na Serikali ya Tanzania,” amesema.