Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikosi kazi chapendekeza ruzuku kwa vyama vyenye usajili, lakini...

Muktasari:

 Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini, kimependekeza kimependekeza vyama vyote vyenye usajili wa kudumu vipatiwe asilimia 10 ya ruzuku inayotengwa kila mwaka wa fedha.

Dar es Salaam. Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini,  kimependekeza vyama vyote vyenye usajili wa kudumu vipatiwe asilimia 10 ya ruzuku inayotengwa kila mwaka wa fedha.

Pia, kimependekeza sheria ya vyama vya siasa itamke kuwa asilimia 20 ya fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa inayotolewa na serikali katika mwaka wa fedha, igawiwe kwa vyama vya siasa vyenye madiwani wa kuchaguliwa katika kata kwa mujibu wa uwiano wa idadi ya madiwani ambao kila chama kinao.

Akiwasilisha mapendekezo hayo leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kikosi kazi, Profesa Rwekaza Mukandala amesema wanapendekeza ruzuku igawiwe sawa kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu.

“Kikosi kazi kinapendekeza mfumo wa sasa wa kugawa ruzuku uendelee, isipokuwa asilimia 10 ya fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa zinazotengwa katika bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha husika, igawiwe sawa kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili kwa mujibu wa vigezo na masharti yafuatayo,” amesema.

Amefafanua ili chama kipate ruzuku hiyo, lazima kiwe na usajili kamili, kiwe kimefanyiwa uhakiki na Msajili wa Vyama vya Siasa na kuthibitisha kinakidhi matakwa na chama kiwe kimeshiriki uchaguzi mkuu angalau mara mbili tangu kimepata usajili kamili.

Vilevile, amesema chama kisiwe kimepata hati chafu baada ya kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) katika mwaka uliopita na ruzuku itumike kwa shughuli za kuendesha ofisi ya makao makuu, ofisi ndogo.

Profesa Mukandala amesema wanapendekeza Sheria ya Vyama vya Siasa itamke kuwa asilimia 20 ya fedha za ruzuku itolewe kwenye vyama vilivyo na madiwani kwa kuzingatia uwiano wa kila chama.

“Sheria ya vyama vya siasa itamke kuwa asilimia 20 ya fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa inayotolewa na serikali katika mwaka wa fedha, igawiwe kwa vyama vya siasa vyenye madiwani wa kuchaguliwa katika kata kwa mujibu wa uwiano wa idadi ya madiwani ambao kila chama kinao, kwani kwa sasa sheria haijatamka kiwango chochote bali imempa mamlaka waziri mwenye dhamana kuamua,” amesema.

Amesema kikosi kazi inapendekeza Serikali iongeze bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa ili baraza hili liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwemo jukumu linalopendekezwa la kusimamia maadili ya vyama vya siasa.