Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kikosi kazi chapendekeza mikutano ya hadhara iruhusiwe

Kikosi kazi chapendekeza mikutano ya hadhara iruhusiwe

Muktasari:

Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania, kimependekeza mikutano ya hadhara iruhusiwe sambamba na mabadiliko ya sheria mbalimbali zitakazowezesha mikutano hiyo kufanyika kwa ufanisi.

Dar es Salaam. Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini Tanzania, kimependekeza mikutano ya hadhara iruhusiwe sambamba na mabadiliko ya sheria mbalimbali zitakazowezesha mikutano hiyo kufanyika kwa ufanisi.

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa, Oktoba 21, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa kikosi kazi, Profesa Rwekaza Mukandala wakati akiwasilisha mapendekezo ya kikosi hicho kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema baada ya kikosi hicho kufanya kazi kwa miezi 10 kikichambua maoni mbalimbali ya wadau, kinapendekeza kwamba mikutano ya hadhara iliyozuiliwa mwaka 2016, iruhusiwe kufanyika.

“Kikosi kazi kinapendekeza mikutano ya hadhara iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa katiba na sheria ya vyama vya siasa. Mikutano ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote.

“Yafanyike marekebisho ya sheria ili kuhakikisha mikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi. Sheria hizo ni pamoja na sheria ya vyama vya siasa sura ya 258, sheria ya jeshi la polisi na huduma saidizi, sura ya 3022 na kanuni za maadili ya vyama vya siasa za mwaka 2019,” amesema Profesa Mukandala.

Mwenyekiti huyo amesema kikosi kazi kinapendekeza Sheria ya Vyama vya Siasa ifanyiwe marekebisho ili kulipatia Baraza la Vyama vya Siasa mamlaka ya kushughulikia uvunjifu wa maadili ya vyama vyenyewe

Pia, kuweka idadi ya jinsi moja ndani ya vyama vya siasa isipungue asilimia 40. Amesema marekebisho hayo yaangazie pia ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu katika shughuli za chama husika.