Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kichanga chatelekezwa Daraja la Kilungule 'A' Kimara

Muktasari:

  • Mashuhuda wamesema waliona mwili wa mtoto mchanga usiku wa kuamkia leo Januari 26, 2024 ukiwa umetelekezwa kwenye Daraja la Kilungule A.

Dar es Salaam. Mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa siku mbili ametelekezwa mtoni katika Daraja la Kilungule A, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam na mtu asiyejulikana, na kusababisha kifo chake.

Mashuhuda ambao ni majirani wa eneo hilo waliozungumza na Mwananchi wamesema wameshangaa asubuhi leo Januari 26, 2024 kuona mwili wa mtoto huyo ukiwa kwenye mto huo.


Mto Kilungule ambao kichanga kinachokadiriwa kuwa na umri wa siku mbili kimetupwa na kupoteza maisha. Picha na Tuzo Mapunda


Hata hivyo, majirani hao wamesema, baada ya taarifa kutolewa polisi, askari walifika na kuuchukua mwili wa kichanga hicho kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

"Ni kweli nimeona mtoto ametupwa kwenye mto huu baada ya jirani yangu kunieleza kuna mtoto, nilipofika nikaona ni kweli ametupwa akiwa hana nguo," amesema Isabela Richard.

Isabela amesema mtoto alikuwa mdogo kama siku mbili tangu kuzaliwa kwake na ni mweupe na jinsia ya kiume na alionekana amepasuka upande mmoja.

Baada ya taarifa kusambaa majirani wengi walifik eneo la tukio hilo na wachache walijitosa kukitoa kichanga hicho kwenye maji na kukiweka pembeni kisha kutoa taarifa kwa mjumbe.

Sehemu alipotupwa mtoto ni kando na nyumba ya Mama Richard, ambaye amesema baada ya kuona tukio hilo walitoa taarifa Serikali za mtaa kabla ya kupiga simu Polisi.

"Walipokuja (askari polisi) tukawaonyesha wakaenda wakamgeuza na kumsafisha na maji akiwa tayari amekwishafariki, kisha wakaondoka na mwili huo," amesema. 

Mkazi mwingine wa mtaa huo, Mariam Selemani amesema aliyetekeleza tukio hilo ana ujasiri wa ajabu kwa kuwa ni la kusikitisa.

"Mama kavumilia miezi tisa kumlea mtoto tumboni lakini anakuja kumtupa kwenye mto. Wakati kila siku tunasikia watu wanatafuta watoto, si haki hata kama mume wake alikataa kulea," amesema Mariam.

Naye Rajab Taslima amesema hilo ni tukio la pili kutokea la mtoto kutupwa katika mto huo, baada ya lile la mwaka jana la mwingine kutupwa akiwa kwenye kikapu.

"Ni mtindo ulioanza kuzoeleka na kuonekana kawaida kwa watu kutupa vichanga kwenye huu mto na wanakuja kutupa usiku, mnashangaa asubuhi kuona mtoto katupwa," amesema Taslima.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilungule 'A' Jumanne Isakwi amesema bado hawajamjua aliyetupa mtoto huyo.

"Mto huu unatenganisha kata mbili za Kimara na Saranga, kwa hiyo kujua nani amefanya ni ngumu kutokana na wingi wa watu, labda tupate taarifa za siri," amesema Kwisa.

Kwisa ambaye pia ofisi afya na mazingira amewasihi wanaweka kuweka ulinzi kuhakikisha matukio ya kutekelezwa watoto yanakoma.

"Matukio ya kutelekeza wa wototo ni mengi kwa miaka tofauti na unajua akina mama ni majasir,i anaweza kutoka upande wa pili kuja kutupa (mtoto) na usimjue, labda majirani waseme," amesema Isakwi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi amekiri kutokea tukio hilo na kuwa wanafutilia kwa kushirikia na viongozi wa mitaa kubaini mtu aliyetelekeza kichanga hicho.

"Ni kweli tukio hilo limetokea na tunaendelea kufuatilia kujua nani aliyetelekeza kichanga hicho," amesema Kitinkwi.