Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kauli ya Serikali Watanzania waishio Afrika Kusini

Wakazi wa Jiji la Durban, Afrika Kusini, wakipita katika Soko la Nguo la Warwick lililopo katikati ya CBD ya jiji hilo. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Wizara ya Mambo ya Nnje imesema hakuna Mtanzania aliyeshambuliwa Afrka Kusini.

Dar es Salaam. Wakati sekeseke la matukio ya mashambulizi ya chuki dhidi ya wageni wanaotoka mataifa mbalimbali ikipamba moto nchini Afrika Kusini, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje imesema hakuna Mtanzana aliyekumbwa na masaibu hayo.

Picha na video zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii kwa siku kadhaa sasa zikiwaonesha makundi ya watu wanaopinga wahamiaji wakiwashambulia na kuwasakama raia wa kigeni walioko nchini humo zimegonga vichwa vya habari na kuibua mijadala pamoja na hisia mseto mitandaoni.

Kupitia taarifa yake ya leo Jumatayu, Aprili 27, 2026 iliyochapishwa kwenye mitandao yake rasmi Wizara ya Mambo ya Nje imeeleza hakuna raia wa Tanzania anayeishi Afrika Kusini aliyeshambuliwa kutokana na ghasia dhidi ya wageni nchini humo.

“Wizara inauhakikishia umma wa Watanzania kuwa picha mjengeo (Video clips) zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikionesha raia wa Tanzania akishambuliwa nchini Afrika Kusini ni upotoshaji unaofanywa na watu wenye nia ovu.

“Picha hizo zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii ni za mwaka 2023 na zimehaririwa upya na watu wenye nia ovu na kuzihusanisha na matukio ya sasa yanayoendelea nchini humo,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umefanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya za Watanzania katika majimbo tisa na kuhakikishiwa hakuna Mtanzania aliyeshambuliwa kutokana na uraia wake wa kigeni.

“Wizara inatoa rai kwa waandaa maudhui mitandaoni kuhakikisha kuwa wanakuwa na taarifa sahihi kabla ya kusambaza katika mitandao, ili kuepuka kuzusha taharuki zisizo za lazima kwa jamii.

“Ubalozi wa Tanzania unaendelea kushirikiana na mamlaka husika nchini Afrika Kusini kuhakikisha kuwa Watanzania nchini humo wanaendelea kulindwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za kimataifa,” imesema.

Kwingineko kwa mujibu wa Shirika la Habari la DW, Serikali ya Afrika Kusini imeahidi kuwasaka wote wanaohusika na matukio hayo ya mashambulizi ya chuki dhidi ya raia wa kigeni.

Taarifa hiyo imetolewa na wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo baada ya kusambaa video hizo, huku ikisema uhalifu unaowalenga wahamiaji ni kitisho kwa utulivu na misingi ya utawala wa sheria ya nchi hiyo.