Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamba za plastiki kutoka nje kupigwa marufuku nchini

Muktasari:

  • Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaangalia utaratibu wa kuzuia kamba za plastiki zinazoingizwa nchini ili kulinda viwanda vya ndani na mazingira.

Tanga. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaangalia utaratibu wa kuzuia kamba za plastiki zinazoingizwa nchini ili kulinda viwanda vya ndani na mazingira.

Amesema unafanyika uchambuzi wa aina gani ya plastiki ianze kuzuiwa na zipigwe marufuku kwa sababu hapa nchini zinazalishwa kamba za aina zote za mkonge ambazo zikitumika na muda wake ukiisha zinaoza.

Majaliwa aliyekuwa ziarani mkoani hapa kutembelea mashamba ya mkonge na kukagua viwanda vya kuchakata na kuzalisha bidhaa zitokanazo na mkonge, alitoa ahadi hiyo alipokuwa katika kiwanda cha kutengeneza kamba cha Amboni Spinning Mills kilichopo Pongwe jijini hapa.

“Tutapitia upya kuangalia uingizaji wa kamba za plastiki kutoka nje ambazo zikitumika zikitupwa haziozi, wakati tuna viwanda vinavyozalisha kamba za mkonge na zimerundikana ghalani kwa kukosa masoko...tumehamasisha kilimo cha mkonge ni lazima pia viwanda vinavyozalisha bidhaa zitokanazo na mkonge tuvilinde” alisema Majaliwa.

Kuhusu viwanda vya kutengeneza magunia vilivyopo nchini, Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali ni kuona msimu wa mavuno mazao mbalimbali ikiwamo korosho yanahifadhiwa na magunia ya mkonge yaliyotengenezwa na viwanda vya ndani.

“Katika hili tungependa kuona viwanda vya ndani vinazalisha magunia yenye kutosheleza mahitaji ya pamba, korosho, chai, kahawa, mahindi na maharage kwa sababu hamasa ya kulima mkonge imeongezeka,” alisema Majaliwa.

Meneja wa kiwanda cha Amboni Spinning Mills, Robert Semwaiko alisema licha ya kuzalisha kamba ndogo na kubwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwamo kuvutia magari, meli lakini bidhaa hizo zimejaa ghalani kwa sababu soko la ndani ya nchi limevamiwa na kamba za manila kutoka nje.

Alisema kamba za manila zina athari katika utunzaji wa mazingira kwa sababu zinapotupwa haziozi, tofauti na za mkonge ambazo huoza na kugeuka kuwa mbolea ya kurutubisha udongo.