Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamati yataka barabara zijengwe kwa kushirikisha sekta binafsi

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Seleman Kakoso akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwenye hotuba ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2023/24 leo Jumatatu Mei 22, 2023 bungeni jijini Dodoma. Picha na Merciful Munuo

Muktasari:

  • Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeishauri Wizara ya Ujenzi kutumia mfumo wa wawekezaji binafsi (PPP na EPC + F) kama ina nia kweli ya kukamilisha ujenzi wa barabara.

Dodoma. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeishauri Wizara ya Ujenzi kutumia mfumo wa wawekezaji binafsi (PPP na EPC + F) kama ina nia kweli ya kukamilisha ujenzi wa barabara.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Seleman Kakoso amesema ili kuwezesha barabara nyingi kujengwa kwa wakati na ubora unaotakiwa, hakuna namna nyingine isipokuwa Serikali kuingia mkataba na sekta binafsi.

Kakoso ametoa wazo hilo leo Mei 22, 2023 wakati akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwenye hotuba ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2023/24.

Hata hivyo Kakoso ameagiza katika mikataba ya ujenzi wa barabara, Serikali iongeze kipengele kitakachofanya mkandarasi na mhandisi mshauri kuongeza muda wa kuendelea kufuatilia na kukarabati barabara zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kuzikabidhi.

“Wakandarasi huchelewa kukamilisha miradi kwa wakati na kuongeza gharama, tuongeze vipengele wa ufuatiliaji na kipengele cha kuzuia ongezeko la gharama,lakini ishughulikie malalamiko ya uwepo wa vituo vya mafuta ndani ya hifadhi ya barabara,” amesema Kakoso.

Amependekeza wakandarasi wanaochelewesha miradi kutokamilika kwa wakati, watoe tozo kuilipa Serikali kwa ucheleweshaji huo kwani itasaidia kuwepo kwa utekelezaji wa muda unaotakiwa.

Kuhusu madeni, amesema kumekuwa na ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi na kutaka kuwepo kwa usimamizi wa taasisi zake ili zilipe madeni kwa Temesa kutokana na huduma wanazopata.

Kwa upande wa reli ya mwendo kasi (SGR), kamati imetaja kuchelewa kufika kwa mabehewa ya treni ikilinganishwa na lengo lililowekwa la Februari, 2022 kwamba ni tatizo lingine.