Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT yawatoa hofu walioitwa kwa mujibu wa sheria

Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga la Taifa (JKT), Brigedia Jenerali Hassan Mabena

Muktasari:

  • Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetoa ufafanuzi wa tuhuma zilizozua taharuki kwenye mitandao ya jamii.

Dodoma. Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajabu Mabele amewatoa hofu wazazi, walezi na vijana kuwa JKT ni mahali salama ambapo watalelewa vizuri kimaadili kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na nchi.

Kauli hiyo inakuja kufuatia wito wa vijana wote wa waliohitimu kidato cha sita mwaka 2013 kutoka shule za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria kwa mwaka 2023.

Mkuu wa Tawi la Utawala la Jeshi hilo, Brigedia Jenerali Hassan Mabena wakatu akizungumza leo Ijumaa Juni 2, 2023 kwa niaba ya Meja Jenerali Mabele.

“Kufuatia wito huo hivi karibuni kumezuka taharuki kubwa katika mitandao ya kijamii kutoka kwa baadhi ya watu wenye nia ovu wasiolitakia mema Taifa letu na kutaka kudhoofisha mafunzo ya JKT,”amesema.

Amesema watu hao wanawatia hofu wazazi, walezi na vijana waliopangiwa kuhudhuria mafunzo kwenye kambi mbalimbali kutokwenda kwa kile kinachodaiwa kuwa mafunzo ya JKT ni mateso, yana unyanyasaji na udhalilishaji hususan kwa vijana wa jinsia ya kike.

Amewataka wazazi, walezi na vijana kupuuza taarifa hizo za uzushi kwa sababu mafunzo hayo ni muhimu kwa ustawi wao na kwa Taifa kwa ujumla.

Amesema mafunzo hayo na yale ya kujitolea yamelenga kumjengea kijana wa Kitanzania uzalendo, ukakamavu, nidhamu na kuleta umoja wa kitaifa.

“JKT katika kuhakikisha vijana hao wanakuwa salama wakati wote, makambi na vikosi vyote vya JKT vina baba na mama mlezi ambao wamewekwa mahususi ili kusimamia ustawi wa vijana wa kiume na wa kike kwa kipindi chote wanapokuwa makambini,”amesema.

Brigedi Jenerali Mabena amesema endapo ikibainika kuna mkufunzi anakwenda kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa za miongozo na malezi ya vijana ndani ya JKT, hatua kali za kinidhamu na kisheria huchukuliwa dhidi yake.

Amewasisitiza vijana wote walioitwa kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka 2023 kuripoti makambini kwa tarehe zilizopangwa.