Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jambo la kuzingatia kuepuka udukuzi mtandaoni

Muktasari:

  • Mtaalamu wa Usalama Mtandaoni, Roshan Pyar amesema kama mtu anasaka ajira au fursa za masomo na nyinginezo kupitia kiunganisho cha ‘http’ aepuke kwa kuwa hao ni wadukuzi kwa njia ya mtandao.

Dar es Salaam. Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao na unasaka nafasi za ajira, kaa chonjo kwa kuwa wadukuzi kwa njia ya mtandao wanatumia matangazo hayo kufanikisha uhalifu.

Mbali na hao, wanaopakua nyimbo kwenye simu au kompyuta wanapaswa kuchukua tahathari kwa kuwa nyimbo hutumika kuingiza virusi hatarishi kwenye vifaa hivyo.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Roshan Pyar ambaye ni mtaalamu wa usalama mtandaoni amesema, muhalifu humtumia mtu kiunganishi (link) inayohusisha nafasi ya ajira au masomo kumbe ni mtego wa kudukua taarifa.

“Unaweza ukawa na wimbo kwenye simu lakini ikawa ni hatari hivyo unapopakua na kuusikiliza ndipo mtu huyo anachukua taarifa zako.

“Kinachofanyika wahalifu mtandaoni wanatumia kiunganishi chenye upungufu ili wawapate walengwa, mara nyingi kiunganishi halisi tunatumia ni https kwasababu ipo salama kwa mtumiaji, kwa mhalifu wa mtandao hawezi kutumia hiyo, anachofanya ni kutengeneza http ambayo haina ‘s’ na kwake itakuwa rahisi kumlaghai mtu kwa kuwa ni ngumu kuzitofautisha kwa haraka,” amesema

Pyar amesema mtu anavyoibonyeza kiunganishi hicho kilichoanza na http humpa muhalifu njia rahisi ya kudukua taarifa zake.

Amefafanua simu peke yake ina ulinzi binafsi ambayo ina mzuia mhalifu wa mtandao kufanya udukuzi hivyo mtu asipobonyeza kiunganisho anachopewa ni ngumu kushambuliwa.

Amesema mtu anayefanya uhaifu mtandaoni huchukua taarifa za mtu na kuzitumia kwa lengo la kudhalilisha, au kutafuta fedha.

“Aina nyingine ni kutumia udhaifu wa mtu kwenye mtandao kumshambulia, mfano nikakuona unatafuta ajira, nikatengeneza kiunganisho (link) nikaweka nembo ya shirika fulani na kuonyesha nafasi za ajira, unabobonyeza unakwenda kwa mtu mwenye lengo la kutekeleza uhalifu dhidi yako, sasa unapoingia unamuachia email yako na namba ya siri,” amesema.

Amesema pale mhalifu anapofanikiwa kupata taarifa hizo za muhimu na nyinginezo hutekeleza uhalifu ndani ya muda mfupi.

Pyar ameshauri jamii kutofungua viunganisho vya nafasi za masomo ajira au vitu vingine bila kujiridhisha na usalama wa kiunganisho chenyewe.

“Ikitokea umepokea barua pepe inayoonekana imetoka kwa mtu unayemfahamu, kuwa makini kabla ya kufungua viambatisho vyake. Ni vema ukiwa na shaka uchukue tahadhari au kutojibu barua pepe husika kwa sababu utambulisho wa mhusika unaweza kuwa umedukuliwa,”amesema.

Watumiaji wa Internet mpaka sasa

Kwa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhusu mwenendo wa sekta ya Mawasiliano katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2023 kumekuwa na ongezeko la watumiaji wa Intaneti kwa asilimia 1.24 kutoka watumiaji 34,047,407, Juni 2023 hadi kufikia 34,469,022 Septemba 2023.

Mpaka sasa matukio mengi yaliyoripotiwa kwa robo ya pili (Aprili - Juni) ya mwaka 2023 ni matukio ya ulaghai ambayo yameongezeka hadi kufikia 23,048.

Hadi Machi 2023, kulikuwa na matukio ya ulaghai wa mtandaoni 12,044 tu.

Hivyo, kwa mujibu wa takwimu hizo ndani ya kipindi cha miezi mitatu matukio mapya 11,004 ya ulaghai wa mtandaoni yalifanyika ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 47.7.

Utapeli kwa njia ya simu ndio umeonekana kuongezeka zaidi na TCRA inaonyesha kwa robo ya pili (Aprili - Juni) ya mwaka 2023 matukio ya ulaghai yameongezeka na kufikia 23,048 ambapo hadi kufikia Machi 2023, kulikuwa na matukio ya ulaghai wa mtandaoni 12,044.