Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hukumu ya aliyekuwa RC Simiyu kutolewa leo

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (RC), Dk Yahya (kushoto) Nawanda wakati akiwasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Ilemela, Mwanza.

Muktasari:

  • Julai 11, 2024, Rais Samia Suluhu Hassan alitengua nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Nawanda, huku nafasi yake ikijazwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, Kenan Kihongosi. Dk Nawanda alikuwa kwenye nafasi hiyo tangu Julai 2022.

Mwanza. Hukumu ya kesi ya kulawiti inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (RC), Dk Yahya Nawanda inatarajiwa kusomwa leo Ijumaa Novemba 29, 2024, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.

Kesi hiyo ya kulawiti namba 1883/2024, inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Erick Marley.

Mara ya mwisho kuripoti mwenendo wa kesi hiyo ilikuwa Septemba 10, 2024 baada ya kutopata ushirikiano licha ya Marley kuruhusu wajulishwe mwenendo wa kesi bila kuvunja taratibu kwa kuwa kesi hiyo ilikuwa ni ya nyuma ya kamera.

Aliyekuwa RC Simiyu mahakamani

Siku hiyo shauri hilo lilitakiwa kuendelea na usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa mshtakiwa (Dk Nawanda).

Kabla ya ushahidi wa upande wa mshtakiwa kuanza kutolewa, Julai 16, 2024 mbele ya Hakimu Marley, mashahidi wawili wa Jamhuri ambao ni mwanafunzi anayedaiwa kulawitiwa na Dk Nawanda na mama mzazi wa mwanafunzi huyo walifungua ukurasa wa kutoa ushahidi ambapo waliutoa nyuma ya kamera (faragha).

Kesi hiyo iliitwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo, Julai 9, 2024, mbele ya Hakimu Marley ambapo mshtakiwa alikana shtaka hilo baada ya kusomewa maelezo ya awali (PH) na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Magreth Mwaseba.

Dk Nawanda anadaiwa kutenda kosa hilo Juni 2, 2024, katika maegesho ya magari yaliyoko eneo la Rock City Mall wilayani Ilemela, Mkoa wa Mwanza kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16.


Endelea kufuatilia Mwananchi