Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hukumu na sharia za usimamizi wa ndoa


Muktasari:

  • Uislamu umeipa umuhimu mkubwa ndoa, umeitukuza na kuilinda, kwa upekee wake na umuhimu wake; kwani unahusiana na heshima za watu, nasaba na kuendelea kwa kizazi cha binadamu.

Dar es Salaam. Mkataba wa ndoa ni miongoni mwa mikataba ambayo Uislamu umeipa umuhimu mkubwa, umeitukuza na kuilinda, kwa upekee wake na umuhimu wake; kwani unahusiana na heshima za watu, nasaba na kuendelea kwa kizazi cha binadamu.

Ikumbukwe athari za ndoa haziishii kwa mwanamke peke yake, bali zinavuka hadi kwa familia yake na jamii yake.

Hivyo, wanazuoni wengi wameweka sharti la kuwepo kwa msimamizi (walii) katika mkataba wa kufunga ndoa kwa sababu ya maslahi mbalimbali yaliyomo ndani yake.

Kuna wanaoona kuwa walii ni nguozo katika usahihi wa ndoa, hivyo ndoa haifungwi bila ridhaa ya walii, na kuna wanaoona kuwa si nguzo bali ndoa hufungwa kwa kauli ya mwanamke mwenyewe. 

Hata hivyo, ni lazima amuombe ridhaa na kumshauri mwanamke, na hana haki ya kumzuia au kumdhuru.

Miongoni mwa ufafanuzi mzuri zaidi wa maana ya msimamizi katika mkataba wa ndoa (walii) ni wa Awadh al-Awfi: Ni mamlaka ya Kisharia kwa jamaa wa nasaba wa upande wa baba au wanaochukua nafasi yao, kwa ajili ya kumwozesha yule ambaye hastahiki kufunga ndoa mwenyewe.

Usimamizi katika mkataba wa ndoa (wilaya) upo wa aina mbili: Mosi. Usimamizi wa ulazimashiji (Ijbaar). Huu ni usimamizi ambao walii ana mamlaka ya kufunga ndoa bila kuomba idhini ya yule aliye chini ya huduma na ulinzi wake.

Wanazuoni wametofautiana kimitazamo kuhusu nani anayekuwa na mamlaka ya usimamizi huu. Kwa mujibu wa madhehebu yetu ya Kishafi baba mzazi na babu mzaa baba wao peke yao ndio wenye mamalaka ya kumlazimisha mwanamke bikira asiyeweza kupambanua maslahi katika mkataba wa ndoa.

Pili. Usimamizi wa hiari (uchaguzi), ni ambao mwanamke hushirikiana na msimamizi wake (walii) katika kumchagua mume; wala walii hana haki ya kumlazimisha, bali yeye husimamia kufunga ndoa yake na yule anayemridhia awe mume wake. 

Huu ni mtazamo wa Jopo la wanazuni (madhehebu matatu Malik, Hanbali na Shafi). Usimamizi huu wa ndoa (wilaya) ya hiari husimamiwa na mawalii (wasimamizi) wengine wasiokuwa wale wenye usimamizi wa kulazimisha. Isipokuwa madhehebu ya Hanafi; kwa sababu kwao mwanamke mwenye akili timamu na aliyebaleghe, awe bikira au aliyeolewa kabla, ana haki ya kujifungisha ndoa; lakini inapendekezwa kwake kumkabidhi walii wake (msimamizi wa ndoa) jambo hilo kwa heshima na adabu.

Jopo la wanazuoni (madhehebu matatu) hoja yao ya kutosihi kwa mkataba wa ndoa bila ya kuwepo msimamizi (walii) ni kauli ya Allah Mtukufu: Na mtakapowapa wanawake talaka nao wakamaliza eda yao, basi msiwazuie kuolewa na waume zao endapo baina yao wamepatana kwa wema..” (2:232).

Aya hii tukufu inawakataza wasimamizi wa ndoa (mawalii) kuwazuia wanawake, baada ya kumaliza eda zao, ikiwa wanataka kurudi kwa waume wao wa zamani kwa ndoa mpya. 

Hili ndilo andiko lililo wazi zaidi katika Qur’ani kwamba msimamizi wa ndoa (walii) ana haki pamoja na mwanamke juu ya nafsi yake, na ni juu ya msimamizi (walii) kutomzuia ikiwa ameridhia kuolewa kwa njia iliyo ya kheri.

Kwa upande wa wanazuoni wa madhehebu ya Kihanafi,  wanaona kuwa mwanamke mwenye akili timamu na aliyebaleghe anaweza kufunga ndoa yake mwenyewe na hata ya mwingine; ingawa hilo linakwenda kinyume na lililo bora zaidi. 

Wamejengea mtazamo wao kupitia kauli ya Ibn Abbas kwamba Mtume wa Allah (Rehama na amani ziwe juu yake) amesema: “Mwanamke asiye na mume (ayyim) ana haki zaidi juu ya nafsi yake kuliko msimamizi (walii) wake, na bikira huombwa idhini yake kuhusu nafsi yake, na idhini yake ni kunyamaza kwake.” Kinachoonekana kutokana na maandiko ya pande zote mbili ni kwamba rai ya Jopo la wanazuoni ndiyo iliyo sahihi zaidi; kwa nguvu ya maandiko yao waliojengea hoja na upande wa uthibitisho na maana.

Msamamzi wa mkataba wa ndoa (walii) ana masharti ambayo yanapaswa kutimia ili awe na sifa ya kuwa walii. Baadhi ya masharti haya yamekubaliwa na wanazuoni wote, na mengine wametofautiana kimitazamo.

 Masharti waliokubaliana wote ni awe na akili timamu, balehe, uislamu, utambuzi (rushd), Na masharti waliotofautiana ni uadilifu, hili ni sharti kwa madhehebu ya Kishafi. Kadhalika awe mwanamume na asiwe katika utekelezaji wa ibada ya Hijja au umra.

Wasimamizi (mawalii) katika kufunga ndoa ya mwanamke ni jamaa wa upande wa baba (asaba). Wanazuoni wa madhehebu manne wametofatiana mitazamo yao katika mpangilio wao, nani atangulizwe kuliko mwingine.

 Kwa uipande wa madhehebu yetu ya Kishafi anayestahiki zaidi kumwozesha mwanamke ni baba, kisha babu wa upande wa baba na kuendelea kupanda juu kianasaba, kisha ndugu wa tumbo moja, kisha ndugu wa baba, kisha wana wao kwa kushuka chini kinasaba.  0712 690811