Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii ndio meli ya Mv Mwanza, ujenzi wafikia asilimia 84

Muonekano wa meli mpya ya Mv Mwanza "Hapa Kazi Tu'' inayoendelea kujengwa katika Bandari ya Mwanza Kusini. Utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 84 na unatarajiwa kukamilika na kukabidhiwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Agosti, 2023. Picha na Saada Amir.

Muktasari:

Itakapokamilika, meli ya Mv Mwanza itakuwa ndicho chombo cha usafirishaji kwa njia ya maji chenye umbo mkubwa kuliko vyombo vyote Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikiwa na kimo cha ghorofa nne yenye urefu wa mita 92.6, upana wa mita 17 na uzito wa tani 3, 500.

Mwanza. Kwa wengi, taarifa zinazojulikana kuhusu ujenzi wa meli mpya ya Mv Mwanza “Hapa Kazi Tu” ni kwamba mradi huo umefikia asilimia 84 huku ikitarajiwa kukamilika na kukabidhiwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Agosti, mwaka huu.

Kwa hakika, huo ni ukweli usiopingika kuhusu meli hiyo ndio itakuwa kubwa kuliko meli zote Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 1, 200, tani 400 za mizigo na magari 20, kati ya hayo, matatu yakiwa ni magari makubwa.

Hata hivyo, yapo mengi yasiyofahamika kwa wengi kuhusu meli hiyo itakayofanya safari katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Mataifa mengine ya Ukanda wa Afrika Mashariki, hususan Kenya na Uganda.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL), Eric Hamisi, meli hiyo itakuwa na maeneo maalum na mahususi kuanzia ukubwa, madaraja, huduma na burudani kwa abiria wakati wote wa safari.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyetembelea na kukagua utekelezaji wa mradi huo eneo la Bandari ya Mwanza Kusini Juni 14, 2023, Eric amesema hadi sasa, mradi huo umefikia asilimia 84 ya utekelezaji.

Ukubwa na umbo la meli

Itakapokamilika, meli ya Mv Mwanza itakuwa ndicho chombo cha usafirishaji kwa njia ya maji chenye umbo mkubwa kuliko vyombo vyote Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikiwa na kimo cha ghorofa nne yenye urefu wa mita 92.6, upana wa mita 17 na uzito wa tani 3, 500.

Mv Mwanza inayojengwa na mkandarasi kutoka Kampuni ya Gas Entec Ship-Building Engineering na Kang Nam Corporation za nchini Korea kwa kushirikiana na Suma JKT kwa gharama ya zaidi ya Sh111 bilioni itabeba abiria 1, 200, magari 20 na tani 400 ya mizigo.

Madaraja ya abiria melini

Meli ya Mv Mwanza ‘Hapa Kazi Tu’ itakuwa na madaraja tofauti kwa ajili ya abiria kulingana na mahitaji na uwezo wao kiuchumi.

Ndani ya meli hiyo, kutakuwa na daraja la hadhi ya juu (VVIP) lenye uwezo wa kuhudumia abiria wawili, daraja la watu mashuhuri (VIP) litakalobeba abiria wanne, daraja la kwanza litakalohudumia abiria 60 na daraja la biashara llitakalobeba abiria 100.

Kwa mujibu wa Eric, madaraja mengine ndani ya meli hiyo ni daraja la pili litakalotumiwa na abiria 200 na daraja la uchumi litakalobeba abiria 834.

Huduma na burudani safarini

Wakiwa safarini, abiria watakaosafiri kwa meli hiyo licha ya kupata huduma ya vyakula na vinywaji vya aina zote kuanzia baridi na vikali katika mighahawa na baa zilizoko ndani ya chombo hicho kulingana na uwezo na madaraja yao.

Burudani ya ya muziki wa dansi na life band kutoka kwa wanamuziki wa ndani na nje ya nchi ni huduma nyingine itakayotolewa kwa abiria kwa lengo la kufanya safari yao kuwa rahisi na nyepesi.

Lifti yenye uwezo wa kubeba watu 20 kwa wakati mmoja ni huduma nyingine maalum itakaypatikana ndani ya meli hiyo kwa ajili ya abiria wenye changamoto za kiafya na viungo.

Abiria wenye matatizo na dharura za kiafya wawapo safarini watapata huduma ya vipimo na tiba katika Zahanati maalum iliyoko ndani ya meli huku wanawake wajawazito na wanaonyonyesha nao wakitengewa eneo maalum wakati wa safari.

Wanaotaka kufunga ndoa na kufanya sherehe wakiwa safarini ndani ya meli nao watapata fursa kutokana na meli hiyo kuwa na ukumbi maalum ya sherehe na burudani.

Safari za meli

Meli ya Mv Mwanza itafanya safari zake kati ya Bandari za Mwanza, Bukoba na Kemondo kwa upande wa Tanzania ambazo zitanufaisha wakazi, maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Geita, Tabora, Simiyu na Shinyanga ambazo ama zinapakana na Ziwa Victoria au zinaunda Kanda ya Ziwa Kijiografia.

Uwepo wa meli ya Mv Mwanza utatatoa fursa ya usafirishaji wa abiria na mizigo katika mikoa hiyo ya Kanda ya Ziwa ambapo kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL), Eric Hamisi, mizigo ambayo kwa sasa inasafirishwa kwa malori 40 itasafirishwa kwa njia ya maji meli hiyo itakapoanza safari.

Pamoja na mikoa ya Kanda ya Ziwa, Mv Mwanza pia itafanya safari katika Mataifa jirani ya Kenya na Uganda ambako nchini Kenya meli hiyo itatumia bandari ya Kisumu huku kwa Uganda itatia na kungóa nanga katika bandari ya Portbail.