Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hekima, uadilifu, mafanikio havikuachi ukiishi maisha ya kumjua Mungu

Kuna uhusiano mkubwa baina ya maisha ya wanadamu ya kumjua Mungu na mafanikio ndio maana maandiko yanasema, “Mjue sana Mungu ili uwe na amani ndivyo mema yatakavyokujia” (Ayubu 22:21).

Hii inamaanisha kuwa jamii yoyote ya watu ambayo itachagua kumjua Mungu na kuishi katika kanuni, sheria na muongozo wa Mungu ina nafasi ya kufanikiwa sana.

Maandiko matakatifu yanaendelea kuthibitisha kwa kuonesha kuwa, “Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa…” (Mithali 1:7a). Hii ina maanisha kuwa katika kumcha Bwana ambako kunatokana na kumjua Mungu huwapatia wanadamu maarifa sahihi ya namna ya kuishi na hatimaye kufanikiwa.

Maisha ya kumjua Mungu hulisaidia taifa kuwa na watu wenye sifa kadhaa ambazo zinaweza kuwa chanzo kikubwa cha mafanikio kama ifuatavyo;


1. Kumjua Mungu hulifanya Taifa kuwa na watu waadilifu(Zaburi 25:8)

Uadilifu ni neno pana linalomaanisha nidhamu, utu, uaminifu na zaidi kutenda sawasawa na mapokeo na taratibu za jamii husika. Kwa lugha nyingine uadilifu ni kutenda jambo kwa kuzingatia maadili ya kijamii, taifa na mahali husika.

Maandiko yanaonesha wazi namna ambavyo Mungu ni mwenye adili na hivyo kila anayemjua anatakiwa kuishi maisha ya uadilifu. Jamii iliyo na watu waadilifu huwa ni jamiiyenye maadili, upendo badala ya upendeleo, ushirikiano badala ya kutengana na hivyo kuiwezesha jamii na taifa husika kuendelea.

Ili kuwa na taifa lenye watu waadilifu lazima liwe taifa la watu wanaomjua Mungu kwasababu kutegemea katiba, sheria, kanuni na mapokeo ya jamii pekee haitoshi lakini maongozi na hofu ya Mungu inaweza kuwa chachu kubwa ya kuwafanya watu kuishi maisha ya uadilifu.

Kila mwanadamu kuna mahali amewekwa na Mungu na lengo la Mungu ni kuona nafasi aliyomuweka kila mtu inamnufaisha na kumsaidia mtu mwingine, ndiyo maana uadilifu ni jambo muhimu kwa kila mtu bila kujali udogo au ukubwa wa nafasi yake katika jamii na taifa.


2. Kumjua Mungu hulifanya Taifa kuwa na watu wachapakazi (2 Thes 3:10)

Paulo alipowaangalia watu wa Thesalonike akagundua wamekuwa wazembe na wavivu wasiojishughulisha na mambo yao ya kiuchumi na badala yake wanasubiria kupewa chakula cha bure bila kutoka jasho.

Hali hiyo inamfanya Paulo kuwaonya kwa neno la Mungu kwa kusema kuwa, “...Ikiwa mtu hataki kufanya kazi basi asile chakula”. Ni vizuri neno hili liangaliwe vizuri kwasababu mara kadhaa limetafsirika tofauti na kushindwa kufikisha ujumbe sahihi kama alivyokusudia Mtume Paulo. Matumizi ya neno, “Ikiwa mtu hataki kufanya kazi” yanaashiria kuwa kuna watu wanatakiwa kuwa wanafanya kazi na kwa sababu wanazozijua wanaamua kutojihusisha na shughuli za kiuchumi na uzalishaji na badala yake kusubiria maisha ya kubebwa, kusaidiwa na matokeo yake kutengeneza kizazi cha watu wavivu na tegemezi.

Ni utaratibu wa ki Mungu kila mwanadamu kuwa na kazi yake ya mikono ndiyo maana Mungu hubariki kazi ya mikono ya mtu (Kumbukumbu 28:12) na yeye pia Mungu humpa mtu nguvu ili andelee kufanya kazi na kupata mali na utajiri

(Kumbukumbu 8:18).

Kumjua Mungu humpa mtu ufahamu kuhusu maelekezo na maagizo ya Mungu kuhusu maisha ya kazi na hivyo kuwa na watu wachapakazi ambao watawajibikia so kwasababu tu ya maisha yao lakini pia wakitambua kuwa na maagizo ya

Mungu kila mwanadamu kuwa na kazi yake ya mikono na yeye kumbarikia kwa kumfanikisha kupitia kazi hiyo.

Sasa hivi taifa linakumbwa na vijana wanaojishughulisha na kubashiri (betting) na matokeo yake tumekuwa na kizazi kivivu, kisicho na ubunifu kinachosubiriwa mali za ghafla ambazo haziwezi kukisaidia kwa sababu mali ya ghafla hupukutika ghafla pia.


3. Kumjua Mungu hutengeneza taifa la watu watiifu

(Yohana 14:15)

Jamii nyingi kwa sasa zinapitia changamoto ya kukosa utiifu yaani watoto hawana utii kwa wazazi, wananchi hawana utii kwa viongozi wao na kupelekea kuwa na jamii isiyo imara (unstable society).

Mungu alipokuwa akiwafundisha watu wake aliwaonya na kuwaonesha kuwa hawawezi kutaka kuonesha kumpenda Mungu kwa kujitoa na kutoa kwake kama hawawezi kumtii yeye Mungu yaani kuzingatia yale anayoyaelekeza ndipo akasema bora kutii kuliko hata sadaka na dhabihuwanazozitoa (1 Samwel 15:22).

Siku nyingine Mungu alipokuwa akitoa muongozo wa namna watu wake wanatakiwa kuishi aliwaonya waziwazi kuwa wanatakiwa kuwatii wazazi wao bila kujali ikiwa tu wanataka kuwa na siku nyingi za kuishi na zenye baraka na mafanikio duniani (Kutoka 20:12). Pia Mungu alipogundua kuwa wanadamu wamechagua kuongozwa na viongozi wanadamu badala ya Mungu katika kuishi mapenzi ya Mungu bado pia alitoa utaratibu kupitia Mtume Paulo kuwa inatakiwa mamlaka zilizopo madarakani ziheshimiwe.


Mchungaji Dk Mulenda Omary

Askofu Mstaafu TAG – Kigoma Kusini

Mchungaji Kiongozi – City Light Cebter, Matosa Goba. Maombi na ushauri 0673-280229