Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haya hapa mashirika, taasisi zilizochangia zaidi ya Sh10 bilioni

Muktasari:

  • Leo Jumanne, Juni 10, 2025, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amepokea gawio kutoka kwa mashirika na taasisi za umma, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Msajili wa Hazina Tanzania, Nehemiah Mchechu amesema taasisi sita ambazo Serikali inamiliki hisa chache zimeongoza katika orodha ya zile zilizotoa gawio la zaidi ya Sh10 bilioni kwa Serikali.

Wakati huohuo, amesema mashirika saba ya umma ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) yanayochangia asilimia 15 ya mapato yake ghafi katika mfuko wa Serikali, yameingia katika orodha hiyo.

Mchechu ameyataja mashirika na taasisi hizo leo, Jumanne Juni 10, 2025 alipotoa taarifa yake wakati wa hafla ya kupokea gawio kutoka taasisi hizo iliyopewa jina la ‘Gawio Day.’

Amezitaja taasisi hizo ambazo Serikali inamiliki hisa chache zikiongozwa na Twiga Minerals iliyotoa gawio la Sh93.6 bilioni, ikifuatiwa na Airtel Tanzania na Airtel Money iliyotoa Sh73.9 bilioni.

Linalofuata kwa mujibu wa Mchechu ni NMB iliyotoa Sh68.1 bilioni, kisha Puma Energy Tanzania Sh13.5 bilioni, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Sh11.7 bilioni na NBC Sh10.5 bilioni.

Kwa upande wa mashirika yanayotoa asilimia 15 ya mapato yake ghafi, amesema iliyoongoza ni Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliyotoa gawio la Sh181.5 bilioni.

Inayofuata, amesema ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) iliyotoa Sh38.8 bilioni, ikifuatiwa na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) Sh29.8 bilioni, kisha Wakala wa Usajili wa Biasahara la Leseni (Brela) Sh20.4 bilioni.

Mchechu amesema shirika linalofuata ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Sh19.2 bilioni, kisha Shirika la Uwakala wa Meli (Tasac) Sh16.3 bilioni na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (Osha) iliyochangia Sh10.4 bilioni.