Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchechu atoa angalizo kwa mashirika ya umma utoaji gawio

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi waliotoa gawio na michango kwa Serikali zaidi ya Sh10 bilioni kila mmoja kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo Juni 11, 2024.

Muktasari:

  • Mchechu amesema hayo leo Juni 11, 2024 Ikulu, jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya upokeaji gawio kutoka mashirika na taasisi za umma

Dar es Salaam. Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu amesema kampuni na mashirika 10 bora yaliyotoa gawio serikalini ni ambayo Serikali ina hisa chache.

 Amesema mafanikio hayo ni somo ambalo Serikali ina kila sababu ya kujifunza namna taasisi zake zinavyoendeshwa.

Mchechu amesema hayo leo Juni 11, 2024 Ikulu, jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya upokeaji gawio kutoka mashirika na taasisi za umma.

Amesema uwekezaji wa Serikali katika kampuni na mashirika hayo ni Sh3 trilioni. Serikali imewekeza Sh76 trilioni kwenye mashirika na taasisi mbalimbali.

Mchechu amesema mwaka 2019/2020, 2020/2021, na 2021/2022 mashirika ya umma yalichangia Sh255 bilioni, Sh161 bilioni na Sh207 bilioni, mtawalia.

Amesema kampuni na mashirika ambayo Serikali ina hisa chache zilichangia gawio dogo la Sh44 bilioni, Sh147 bilioni na Sh10 bilioni mtawalia.

Mchechu amesema kwa miaka miwili 2022/2023 na 2023/2024 gawio kwa mashirika ya umma yanayofanya biashara lilikuwa Sh109 bilioni na Sh110 bilioni mtawalia; huku ambako Serikali ina hisa chache zilichangia Sh219 bilioni na Sh168 bilioni kwa kipindi hicho.

“Matokeo haya kwetu yanaleta fikra mchanganyiko, ni habari njema kwa kuwa inaonyesha uwezeshaji unaofanywa na Serikali kuendeleza mazingira wezeshi ya biashara, kampuni binafsi inapofanya kazi na kupata faida mazingira ni mema,” amesema Mchechu.

Amesema faida katika biashara ya sekta binafsi ni kipimajoto cha mafanikio ya Serikali kuboresha mazingira ya biashara na sera za kiuchumi.

Mchechu amewataka viongozi waliochaguliwa kuongoza mashirika ya umma kufanya vizuri zaidi kwa faida ya Taifa na wananchi.

“Kama tutazingatia Sh850 bilioni mwaka hadi mwaka inawezekana tukawa na furaha, lakini kama tutaangalia kiwango hiki tunachotoa sasa kwa malengo tuliyopatiwa tukiwa Arusha ya mapato yasiyo ya kikodi yafikie asilimia 10 ya kikodi tupo mbali sana, mwaka jana tulikuwa asilimia tatu na mwaka huu tupo asilimia tatu,” amesema.

Mchechu amesema ni lazima ukuaji uwe wa wastani wa asilimia kati ya 60 hadi 70 ili kufikia malengo ya mapato yasiyo ya kikodi kwa asilimia 10.

“Hali si nzuri kwa sababu bado hatuendani na kasi na maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuleta maendeleo kwa kasi nchini, maen deleo yote yanategemea fedha, chanzo cha fedha ni vitu vitatu, Serikali kukopa, kukusanya kodi au kupata mapato yasiyo ya kikodi. Asilimia 90 ya mapato yasiyo ya kikodi hupatikana kupitia gawio,” amesema.


Gawio lililotolewa

Akizungumzia gawio lililowasilishwa kwenye mfuko mkuu wa Serikali, Mchechu amesema ni Sh637 bilioni, linalojumuisha gawio la Sh279 bilioni kutoka mashirika ya biashara na Sh358 bilioni za taasisi nyingine.

Makusanyo hayo amesema ni kuanzia Julai 2023 hadi Mei 2024, huku kiwango kikitarajiwa kuongezeka mwishoni mwa mwaka huu wa fedha kufikia Sh850 bilioni.

“Nitoe rai kwa wanaodaiwa au wale ambao bado hawajatoa kuhakikisha wanakamilisha malipo kabla ya mwaka wa fedha kwisha,” amesema.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema miongoni mwa mambo wanayosimamia ni mchango wa taasisi kwenye uchumi kuhakikisha unaongezeka na kupunguza mzigo kwa Serikali unaotokana na kuhudumia taasisi hizo.

“Hapa Rais ni pagumu pia kwa sababu ulituelekeza tufanye tathmini ya mashirika ya umma ili yale ambayo yamepitwa na wakati tukushauri uyafute na mengine tuyaunganishe, tumefanya kazi hiyo kwa awamu ya kwanza tunaenda kuunganisha mashirika 16 na mengine manne yanaenda kufutwa,” ameeleza Profesa Mkumbo mbele ya Rais Samia aliyehudhuria halfa hiyo.

Profesa Mkumbo amesema hilo ni gumu kwa kuwa alinyooshewa vidole kuwa anaenda kuua mashirika ya umma.

Amesisitiza mashirika yatakayounganishwa wenyeviti wa bodi ama mmoja atabaki au wote wataondoka na haiwezekani wote wawili wafanye kazi.

“Mashirika hayo ndiyo yanafanya kazi na mashirika binafsi, hivyo kuwa na mashirika ambayo hayaangalii biashara vizuri, mazingira ya biashara yatakuwa magumu,” amesema.